Kulikuwa na tangazo ambalo lilienea sana mitandaoni kuanzia July 28 2015 ikiwa na taarifa kwamba CCM watafanya Kikao chao Makao Makuu Madogo July 29 2015 Lumumba Dar.
Katibu Mwenezi wa CCM Dar, Juma Simba Gaddafi ndio Kiongozi pekee wa CCM aliyefika kwenye Mkutano huo ambao umefanyika Peacock Hotel Dar, na hii ni sehemu ya alichokisema.
‘CCM inatoa shukrani kwa ushirikiano mlioutoa katika Mkutano wetu Mkuu wa Kumtambulisha Mgombea Urais Dk. Magufuli pale Mbagala, CCM ni Chama chenye busara tumeona tuwashukuru‘>>>
Kwenye sentensi nyingine amesema hivi >>> ‘Tume ya Uchaguzi tunawaomba wawe makini kuongeza Mashine na Watendaji ili watu wapate nafasi kujiandikisha na watumie fursa yao Kupiga Kura… CCM tuna uhakika tutashinda‘>>>
Juma Simba Gaddafi, Katibu Mwenezi na Itikadi CCM Dar.
‘Kingine tunawashukuru waliojitokeza Kugombea nafasi mbalimbali za Ubunge na wajitokeze kwa wingi pia kupiga kura… Tumemaliza Uchaguzi Dodoma na kumpata Mgombea wetu Dk. Magufuli, tunajivunia kwa sababu ana rekodi nzuri… Tuna imani CCM itaendelea kuongoza 2015 mpaka 2020, tumefanya mengi yanayokubalika‘>>>
Hiki ndio alichokijibu kuhusu ishu ya Lowassa kuhamia CHADEMA >>> ‘Yeye aliingia CCM kwa ridhaa yake hakuna mtu alimlazimisha, ametoka kwa ridhaa yake na CCM itabaki kuwa CCM… Wafuasi walikuwa ndani ya CCM, kuondoka kwake ameondoka yeye na sio wa kwanza kuondoka‘>>>
Haya ni majibu yake mengine kuhusu Lowassa kutoka CCM >>> ‘Mtu akitoka huwezi kujibu kwa nini ametoka, nawathibitishia mtu yoyote akitoka CCM itabaki imara… Tutashinda asubuhi kweupe… Kama Lowassa angekuwa anaondoka na watu wengi ungewaona jana, lakini alikwenda yeye akarudisha kadi… watu wengi wanatoka kwenye Chama na CCM bado iko imara‘ >>>> Juma Simba Gaddafi.
Vipi hapa...sasa kama wana CCM wakubwa hawakuja ni kwamba wamepinga au nao wanaunga mkono ili nao wahamie CHADEMA au ACT....ngoja tusubiri
ReplyDelete