Tuesday, July 14, 2015

Hii ni hatari sana,kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo(14.7.2015),Ukurasa wa 35,inasema kasi ya vijana kuambukizwa virusi vya Ukimwi ni kubwa,kati ya mwaka 2011 na 2012 vijana wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 24 kwa mkoa wa Dar es Salaam,vijana 40,000 walipimwa na kukutwa wameambukizwa virusi vya Ukimwi,huku mikoa ya Shinyanga,Kagera na Mbeya wakikutwa vijana 10,000,kuna hatari kubwa sana,Dar es Salaam pekee inapokuwa na vijana 40,000 wanaambukizwa ukimwi kwa mwaka,lazima taifa licukue hatua kuwanusuru vijana wetu!kwa mujibu wa Gazeti la mwananchi linasema vijana wetu hawa wanaambukizwa virus hivi na watu wazima wenye pesa zao,huku wakitumia pesa zao kuwamaliza vijana wadogo.

0 comments:

Post a Comment