Saturday, July 18, 2015

Hii ni fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge ya Meya wa manispaa ya ilala anayemaliza muda wake Mhe.Jerry Silaa ambapoa amejiskia mwenye furaha ya kweli baada ya mwananchi wa kawaida amabaye ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa kumfanyia shtukizo(Surprise) na kumletea hela Tsh 120,000 zilizochangwa na wananchi mbalimbali wa ukonga kwa ajili ya kumsaidia mgombea huyo kulipia form yake ya ubunge hapo juzi ambapo amesema imempa moyo na guvu mpya ya kuamini jinsi gani wananchi wa ukonga wanavyomuhitaji awatumikie na kwamba hatawaangusha.....Masama Blog imemnukuu meya Silaa akieleza kuhusu kuguswa kwake na mtu huyu anayejulikana kwa jina la Hamis Gea....Hapa namnukuu Meya Silaa


''Hamis Gea ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ya Nyeburu-Buyuni.
Amekuja kwa ridhaa yake na kunichangia 120,000/- kwa ajili ya fomu ya Ubunge wa Jimbo la Ukonga na nauli ya kwenda wilayani.
Anathami mchango wangu kwenye chaguzi za mitaa na kazi zangu na Jerry Silaa Foundation za kuchonga barabara kwenye Mtaa wake na mitaa mingine.
Lazma nikiri, ingawa tunafanya wajibu wetu lakini hakuna kitu kinachofariji kama mtu akitambua mchango wako.
Asante sana Gea.
Sintasahau hisani yako...

0 comments:

Post a Comment