Kijana Abubakar Ally ‘Babuu’. SIKU chache baada ya nyota wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila, ‘Ray C’ kutangaza anatafuta mchumba, kijana aliyejitambulisha kwa jina la Abubakar Ally ‘Babuu’ (21) amejitokeza akisema yeye anataka ndoa na Ray C.
Ni baada ya kutonywa na vyanzo, mapaparazi wetu walifika eneo hilo na kumshuhudia kijana huyo akizuiwa kuingia hospitalini hapo na mlinzi.
Babuu aliwaomba mapaparazi wetu wamuelekeze nyumbani kwa Ray C baada ya kumkosa kwenye Jengo la Biashara Complex, Mwananyamala.
“Mimi nataka kumuoa Ray C. Amesema kwenye tangazo lake Instagaram kwamba, mwanaume anayemtaka awe tayari kushea naye simu. Niko tayari, tena nitampa mapenzi yangu yote, nisaidieni kunielekeza kwake,” alisema Babuu.
Akaendelea: Nataka nimuoe. Mambo ya umri na pesa si vitu vya kuviangalia kwenye mapenzi.”
huku akiwa na mfuko mweupe ambao alidai ndani yake mlikuwa na barua ya posa na zawadi ya kadi.
Babuu aligonga geti kubwa, msichana mmoja alitoka na kujitambulisha kuwa ni ndugu wa Ray C. Alisema Ray C hakuwepo ndani ya nyumba hiyo.
Ray C alipotafutwa na Amani juzi kutaka kujua kama anafahamu alitafutwa alisema: “Siyo huyo tu. Wamenitafuta wengi sana. sikujua kama ishu itakuwa kubwa hivyo… Teh! Teh! Teh!”
0 comments:
Post a Comment