
OWM-TAMISEMI
inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha
Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015.Wanafunzi waliochaguliwa ni
kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Jumla
ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana31,700
wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.
Wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 wataanza muhula
wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015 na hakutakuwa nafursa ya mabadiliko
yoyote ya shule.
Wanafunzi
wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo
mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya
mwisho yakuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine
aliyekosa nafasi.
Orodha
ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano naVyuo vya
Ufundi mwaka 2015 inapatikana kwenye tovuti ya OWMTAMISEMI
ya www.pmoralg.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu,
0 comments:
Post a Comment