Minong’ono! Tumbo la staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
limezua maswali kwa wadau kibao kama ni la kawaida au tayari mwandani
wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Muziwanda’ ameshampachika ujauzito.
Shilole au Shishi Baby alizua minong’ono hiyo wikiendi iliyopita
nyumbani kwa mwigizaji, Aunt Ezekiel Grayson maeneo ya Mwananyamala
jijini Dar ambapo kulikuwa na shughuli ya 40 ya mtoto wa Aunt, Cookie
iliyokwenda sambamba na futari huku mastaa kibao wakijumuika katika
tukio hilo.
Akiwa kwenye tukio hilo, Shilole alizua maswali baada ya tumbo lake kuonekana limejaa kama mjamzito.
“Dah nipo kitambo sasa lakini sijapata picha kama tumbo la Shilole ni
mimba au kashiba tu, maana kwa uzoefu wangu jinsi anavyoonekana atakuwa
na mimba,” alisema mmoja wa mashuhuda.
Baada ya kuona hali hiyo, mwanahabari wetu alimfuata Shilole kwa
lengo la kumtaka azungumzie ishu hiyo kama ni tumbo tu au ameshanasa
ujauzito, ambapo alisema:
“Ni kweli nina mwanaume rijali lakini sijabahatika kupata mimba,
nadhani muonekano wa tumbo ni kwa sababu ya nguo niliyovaa ila natamani
kupata mtoto,” alisema Shilole.
0 comments:
Post a Comment