ULE
msemo usemao ‘wagombanao ndiyo wapatanao’ umetimia kwa staa wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya kuwa na mgogoro kwa muda
mrefu na baba yake, Abdul Jumaa ‘Baba D’ ambapo anadaiwa kusalimu amri
na sasa wanaelewana, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kukunyetishia.
Chanzo
makini ambacho ni rafiki wa karibu wa Baba D, mapema wiki hii
kililieleza gazeti hili kwamba, kwa sasa Diamond amesalimu amri kwa baba
yake kwani amekuwa akimsikiliza na kumsaidia pale anapokuwa na shida
tofauti na ilivyokuwa awali.
“Angalau sasa Diamond anamsaidia baba
yake kwani hata akimpigia simu anamsikiliza na anampa fedha ndogondogo
za matumizi tofauti na zamani,” kilinyetisha chanzo hicho kwa sharti kuu
moja tu la kutochorwa jina gazetini
0 comments:
Post a Comment