Monday, July 20, 2015

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar wakiwa katika ufukwe wa Coco Beach.
Taswira ya ufukweni.
Ufukwe wa Coco ukiwa umefurika umati wa watu.
Wakazi wa Dar wakiendelea kuponda raha kwa kuogelea na burudani nyingine.

KATIKA kusherehekea Sikukuu ya Idd Pili ambayo huadhimishwa na waumini wa Dini ya Kiislam duniani kote, leo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameonekana kufurika katika Ufukwe wa Coco Beach, uliopo Masaki jijini Dar, huku wengi wao wakijiachia kwa kuogelea na ‘kubarizi’ pembezoni mwa fukwe hizo. 


Wengi waliojitokeza katika fukwe hizo ni watoto na vijana ambao muda wote walionekana wakiwa na furha.
Hapa ni baadhi ya picha zinazoonesha matukio ya wakazi hao wakiwa ndani ya bahari wakiogelea, huku wengine pembezoni.
(Habari/Picha: Denis Mtima/GPL)

0 comments:

Post a Comment