Wake za watu wanaofahamika kama mama Sabra mwenye kigauni kifupi cha draftidrafti, mama Jenifa mwenye kimini cha njano na mama Athuman wakijitoa ufahamu mbele ya mahrusi.
Akina mama watatu ambao ni wake za watu, wanaounda Kundi la Heshima Pesa Shikamoo Makelele lenye maskani yake maeneo ya Mawenzi mjini hapa wanadaiwa kuwachefua baadhi ya watu baada ya kujitoa fahamu na kumwaga ‘lazi’ hadharani na mbaya zaidi mbele ya watoto wadogo
Kwa mujibu wa ‘shujaa’ wetu, tukio hilo la aibu ya aina yake lilijiri juzikati kwenye Ukumbi wa Savoy mjini hapa ambapo wanawake hao walialikwa kuburudisha kwenye sherehe ya harusi ya jirani yao.
.
0 comments:
Post a Comment