Wednesday, July 8, 2015

 Gladness Mallya na Gabriel Ng’osha BAADA ya vuta nikuvute ya wazazi wa wanafunzi, Hilary na Hamis ‘watoto wa Diamond’ walioshinda katika shindano la kucheza Ngololo mwaka jana na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuahidi kuwasomesha katika shule ya East Africa International iliyopo Mikocheni, Dar huku akishindwa kuwalipia ada na watoto hao kurudishwa nyumbani, hatimaye wamerejeshwa tena shuleni.
Baada ya gazeti hili kuripoti habari ya Diamond kushindwa kuwalipia watoto hao ada, limekuwa likifuatilia hatua kwa hatua japokuwa wazazi wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kutosha kutokana na kile kilichodaiwa kwamba watu wa Diamond waliwaambia wafunge mdomo.  


0 comments:

Post a Comment