Dar
es Salaam.Sasa ni rasmi, waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ndiye
mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema.
Mwanasiasa huyo mkongwe na ambaye amekuwa gumzo ndani ya CCM, alikitosa
chama hicho na kujiunga na upinzani.
Baada ya kujiunga na Chadema,
alichukua fomu za kugombea urais na kudhaminiwa na wanachama wapatao 1.6
milioni. Jana alitambulishwa na kupitishwa rasmi na Mkutano Mkuu wa
Chadema pamoja na mgombea wake mwenza, Juma Duni Haji.
Twende kazi mzee UKAWA for change
ReplyDelete