Wednesday, August 26, 2015

Kukosekana kwa Katibu Mkuu katika chama cha UKAWA kumeendelea kuwatesa jana baada ya kwenda kuomba Uwanja wa Jangwani kwa ajili ya kufungulia kampeni zao za Urais na kukuta Uwanja huo ulishakodiwa na mtu mwingine ambaye tayari alishaulipia malipo yake tayari na ushahidi ni hii barua waliyotumiwa UKAWA jana kuhusiana na ishu hiyo. Kinyume na Ukweli kwamba UKAWA wamekuwa wakitangaza kufanya Kikao chao hicho Jumamosi Jangwani huku wakijua wazi kwamba hawakuwa wameomba Uwanja huo mpaka Tarehe 22/8/2015 ndipo walipoenda na kukuta hakuna nafasi. Cha kushangaza ni kuwasikia baadhi ya wafuasi wao wakilalamika kunyimwa Uwanja na huku wanajua kabisa kwamba ukweli ni hawakuwahi kuomba Uwanja huo kama inavyotakiwa.


0 comments:

Post a Comment