1. BUNDA/MUSOMA;- Mgombea wa Chadema aliyeshinda kura za maoni ameamua kujiunga na CCM, baada ya Chama hicho kumpitisha Esther Bulaya kuwa ndio mgombea wake. Pia uongozi mzima wa Chadema Wilaya hiyo umejitoa Uongozi wa Chama hicho kupinga kitendo hicho cha kumpitisha Mgombea aliyetokea CCM majuzi tu!!
2. SIKONGE/TABORA:- Uongozi wa Chadema umeahidi kujiondoa uongozi wa Chama hicho Wilaya hiyo iwapo Chadema itampitisha Said Mkumba aliyetokea CCM na kumuacha mgombea wao aliyeshinda kihalali kura zao za Chadema kwenye maoni.
3. MBARALI/MBEYA:- Mgombea wa Chadema Mbarali Modestus Kilufi leo amejikuta kwenye wakati mgumu alipokwenda na wafuasi wake wa Chadema kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo na kuambiwa kwamba nafasi hiyo imeshachukuliwa na Mgombea wa CUF Liberatus Mwang'ombe. Mgombea huyo amabye hivi karibuni alijiunga na Chama hicho akitokea CCM amejikuta akitokwa na machozi kutokana na uhuni huo aliotendewa na Chadema waliomuahidi kumpa nafasi hiyo.
4. SEGEREA/UKONGA DAR:- Mgombea Ubunge wa UKAWA Julius Mtatiro amejikuta kwenye wakati mgumu sana baada ya kugundua Chadema wana mpango wa kumuweka Makongoro Mahanga kugombea nafasi hiyo bila ya kumtaarifu kuhusu uamuzi huo.

0 comments:
Post a Comment