Sunday, August 30, 2015

Hatimaye zaidi ya wanachama 50 wanaojitambulisha ni kundi la 4U Movement wawasili kituo cha polisi Oterbay jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuripoti malalamiko yao, aidha vijana hao awali waliahidiwa kupewa malipo ya 500,000/= TSH, mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni zinazotarajiwa zilizonyika jana katka viwanja vya Jangwani. Vijana hao
wameambatana na barua za awali zilizotolewa na kiongozi wao. Rejea barua MWININGA, ambaye ni mratibu MPYA WA 4U MOVEMENT KITAIFA.


Wana 4U movement mkoa wa Kilimanjaro na maeneo mengine kama ambavyo tumekubaliana kwenye kikao chetu juu ya kwenda Dar kwenye uzinduzi wa kampeni za Lowassa tutaondoka Moshi mjini saa 12 jioni.

Tutaondokea Mekuz na viongozi wa msafara watakuwa makamanda wetu Fredi Mushi na Paul Matemu tuwahi jamani.

Tumeamua kuondoka muda huo ili tupite usiku kwa usiku wasione kama lowassa ametoa watu mikoani lakini pia tulishakubaliana tutampa kila mtu nauli yake ya daladala ilituingie Jangwani kwa daladala kuwaaminisha watu kuwa tumekwenda kwa mapenzi yetu. Msisahau majina ya hoteli zenu mtakazofikia ukisahau wasiliana na mratibu wako.

Maelekezo mengine mtapewa na viongozi wenu.

By Dr Juma Mwininga 
Mratibu Mpya Wa 4U movement na Team Lowasa Kitaifa.

0 comments:

Post a Comment