Kutokana
na demokrasia kila mtu ana haki ya kumchagua kiongozi ambaye anadhani
kuwa anafaa bila shinikizo la mtu, hii imetokea pia kwa baadhi wasanii
ambao wamegawana katika makundi ambapo kuna baadhi wapo team Lowassa na
wengine team Magufuli.
Hadi sasa kuna baadhi ya mastaa wa Tanzania,
wameweka wazi watu wanaowakubali kati ya wagombea wawili, miongoni mwao
ni Wema Sepetu aliyeweka wazi kumsupport Magufuli, muigizaji Jacqueline
Wolper na Aunty Ezekiel wanamsupport Edward Lowassa na sasa ni Diamond
ameweka wazi kuwa yupo team Magufuli.
Kupitia mtandao wa kijamii
Diamond ameandika “Iwe Msanii, Mtangazaji, ama Mwanamichezo, ila Kila
Mtanzania anahaki ya Kuchagua kiongozi anaeamini ni Bora, Mchapa kazi,
Mwenye Afya na Msimamo ili kutuendelezea Nchi yetu… Kwa Uchunguzi na
tathmini niliyoifanya tangu hizi mambo za Kampeni zianze nimegundua na
kuamini kuwa huyu ndio Jembe,”.
Akamalizia “Nitakuandikia na
kukupostia ushahidi kukuthibitishia kwanini nimeona John Magufuli Pombe
ndie anaefaa… unapohisi na wewe una fact za kumtetea umtakaye karibu
uniambie hapo halaf na mi nikumwagie zangu, ila usijisumbue Matusi coz
hayatokusaidia wala kunisaidia kunibadilisha akili yangu kwa sababu
sanasana ntakuona Huna akili Maana nishayazoea, nipe fact zako nami
nikupe zangu ili pamoja Tujenge nchi….. #HapaKaziTu #Ccm,”.

0 comments:
Post a Comment