Akipiga
stori na Amani, Esha alisema kuwa kuna mambo mengi yamekuwa yakimkwaza
kwenye tasnia hiyo likiwemo suala la malipo, isitoshe tasnia ya filamu
imeshuka kwa kuwa kazi nyingi sokoni zinagongana zikiwa na ladha moja ya
mfumo wa maigizo.
“Nimeamua
nijikite kwenye biashara, naanza kwa kufungua mgahawa na tayari
nimeshapata wadhamini. Kwenye sanaa kuna vitu vingi nimevivumilia lakini
nilichoambulia labda ni kushushwa thamani tu kwa kile kinacho
onekana wasanii hatujatulia,” alisema Esha.
0 comments:
Post a Comment