MIRIAM
Jolwa, maarufu kama Jini Kabula, ambaye ni staa kutoka Bongo Movie,
amemshangaa aliyekuwa mpenzi wake, Ruta Bushoke kumkana kuwa hawajawahi
kuwa wapenzi.
Akistorisha
na gazeti hili hivi karibuni, Kabula alisema maneno ya mkali huyo wa
muziki wa Kizazi Kipya yanaashiria kama mtu anayechanganyikiwa, kwani
asingeweza kujinadi kuwa ni mpenziwe kama haikuwa hivyo.
“Yaani
inawezekana Bushoke anataka kupata uchizi kwa kweli, hivi kuna mtu
anaweza kujinadi kuwa ni mpenzi wa mtu wakati siyo! Kwanza kwa kitu gani
jamani? Nina wasiwasi naye kwamba siyo mzima,” alisema Kabula.
Wiki
chache zilizopita, Bushoke aliyeimba kibao cha Mume Bwege, aliwahi
kudai kuwa hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Jini Kabula.
0 comments:
Post a Comment