Aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Chiligati, amewapiga kijembe makada wanaohama CCM na kujiunga upinzani kuwa ni magamba yanayojivua yenyewe na kukiacha chama hicho kikiwa kisafi na kinachosimamia misingi yake ya kujali wakulima na wafanyakazi.
Samia Suluhu Hassan, katika Jimbo la Manyoni Mashariki jana, Chiligati alisema CCM miaka ya nyuma iliwahi kuwataka makada waliokuwa na kashfa mbalimbali ambayo walipewa jina la magamba wajiondoe wenyewe na kwamba sasa ndiyo kazi hiyo imeanza kufanyika.
Chiligati ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki na ametangaza kustaafu siasa, alisema baada ya magamba hayo kujivua na kumalizika, CCM kitabaki kuwa cha wafanyakazi na wakulima kama kilivyokuwa tangu kinaasisiwa.
Alisema CCM kina wanachama zaidi ya milioni saba lakini kuna watu wachache wanakiharibia sifa yake nzuri na kuonekana kama chama cha mafisadi na kimetekwa na watu wenye fedha nyingi.
Samia aliahidi kwamba ikiwa chama hicho kitashinda uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu, serikali yake itajenga kiwanda cha chokaa katika jimbo hilo ili kiweze kutoa ajira kwa vijana.
Pia aliahidi ujenzi wa barabara mbalimbali, kutatua matatizo ya maji na kulipa fidia wananchi ambao ardhi yao ilichukuliwa na serikali kwa shughuli mbalimbali bila kulipwa.
Samia aliahidi kwamba CCM kikishinda kitaendelea kujenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali. Akiomba kura kwa wananchi, mgombea ubunge wa Jimbo la Manyoni (CCM), Yahaya Masare, alisema jimbo hilo lipo nyuma kimaendeleo lakini yeye amejipanga kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi.
Alisema shida ya maji katika jimbo hilo ni kubwa na kuwaahidi wananchi kwamba atashughulikia tatizo hilo ili kulimaliza.
0 comments:
Post a Comment