Ni napenda kuungana na watanzania wote hususani wanachama wa vyama vinavyounda
UKAWA ambao wengi wao wamestushwa, kukerwa na kushangazwa na kile
kilichofanywa na viongozi wa UKAWA ambacho kimeonyesha wazi kuwa umoja huo
hauna uzalendo KWA Taifa bali viongozi waliopo katika umoja huo wamejawa uchu
ulioanikwa na viongozi hawa hawa wa Ukawa juu ya edward Lowassa? Hali hii
imenifanya naamini kuwa kwa sasa siasa imevamiwa na maharamia.
LAKINI NINI KINAMSUKUMA LOWASSA KUSAKA URAIS HATA KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA?
KATIKA uhalisia ni wazi kuwa Lowassa ametumia pesa nyingi KATIKA mchakato wa
Uchaguzi kuliko hata gharama ya kuendeshea TUME ya Uchaguzi. Je pesa hii
aliitoa wapi?
Duru za uhakika zinasema pesa hiyo ilichangwa na wa fanya biashara wakubwa
nchini, makampuni makubwa nje ya Nchi, na Nchi za kigeni zenye uchu wa kuunda
mikataba ya kuchuma raslimali mbalimbali humu nchini. Makubaliano ya kutolewa
pesa hiyo ni kwamba Lowassa atakapo fanikiwa kushinda watu hao watapewa fursa
za uwekezaji na makampuni kadhaa yatasamehewa kodi huku Nchi kadhaa zikiahidi
kutoa misaada mdogo mdogo KWA wananchi kwa tenda za "Dili" za Serikali. Hali
hii ni hatari sana kwa wananchi wa hali ya chini.
KWANINI LOWASSA KAHAMIA CHADEMA?
Kuhamia kwa Lowassa CHADEMA tunaweza kusema ni haki yake kikatiba lakini
uhalisia ni kwamba Shinikizo kutoka kwa watu waliowekeza kwa Mgombea huyu KWA
kutoa mabilioni ya fedha ndio kunamfanya agombee kwani wafadhiri wa harakati
hizo wamegoma kumuelewa kabisaa Lowassa kwani aliwahakikishia kuwa lazima
atapitishwa na CCM hivyo kuwa fanya wamwage pesa wakijua wazi wanapalilia
"deal".
Baada y kukatwa kwa Lowassa ndani ya CCM wawekezaji hawa KATIKA siasa
walishinikiza kurejeshewa pesa zao lakini Mzee Lowassa asingeweza kuwa
rejeshea pesa hiyo. Kilichofuata yalikua mazungumzo kati ya Lowassa na CCM
akiwaomba basi wamsaidie kulipa mabilioni hayo ya Pesa lakini Chama cha
Mapinduzi kilisema KWA msimamo kuwa hakitolipa Pesa hiyo na hakuna sababu ya
kulipa Pesa isiyo na manufaa kwa watanzania. Sasa hali ilikua ngumu baada ya
baadhi ya wafadhiri kuamua kumfirisi Lowassa au kumtaka ajitose KWA gharama
yoyote kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais kupitia upinzani. Hii INA maana
Lowassa ameingia upinzani kwa shinikizo la Wafadhiri wake ili kutetea maslahi
ya Wafadhiri hao.
Hapo nadhani watanzania tuwe wazalendo kwa Taifa, pingeni kwa uwazi ujio wa
Fisadi LOWASSA katika kivuli cha UKAWA. Ninawapongeza wana Ukawa wanaozidi
kustukia mchezo kila dakika iendayo kwa Mungu. Tuungane kutetea raslimali
mbalimbali za Nchi Yetu, tusikubali kuuza Nchi Yetu.
Josias Charles @2015
Hujielewi wewe! kinachomsukuma ni kutaka kulitumikia taifa hili basiii! halafu hata kama viongozi wa upinzani walimsema saana hiyo siyo shida maana si alikua adui yao!? sasa ulitaka wamrembe!? lakini sasa ni UKAWA lazima wampongeze kwa hatua aliochukua bwanaaaa. kama unamuona ana makosa mpeleke mahakamani!!
ReplyDeleteHivi hao ccm wana huruma gani na nchi hii hadi kushindwa kumlipia Lowasa!! Halafu hivi wewe unawaona UKAWA pumba sana eh!? yaani bila kumchunguza Lowasa agenda zake wampe nafasi kubwa kama ile lo!! acha uzandiki na kutapatapa wewe!!
ReplyDeletetulia wewe msema kweli utaujua ukweli tu picha ndio linaanza hahahaha
ReplyDeleteMh! Mwandishi nikiisoma makala yako naona ipo kishabiki zaidi kuliko uhalisia
ReplyDeleteJe! Unao ushahidi wowote juu ya hizi tuhuma? Kama ushahidi upo naomba weka bayana ili nasisi kama wasomaji tupate nguvu ya kutia kura halali, na sio ushabiki na mawazo hasi ya vyombo vya babari.
Pia ukiandika makala kuwa makini na kutambua wakati gani utumie herufi "R" au "L"