Kauli ya Juma Volter Mwapachu Kuhusu Lowassa
Nimekuwa
kimya kwa muda mrefu katika mabadilishano ya fikra kwenye mtandao huu
ambao kwa hakika, kwa maoni yangu, haubidi kuwa ni wa fikra pevu zisizo
shawishika na misimamo ya 'kimalaya ya siasa'.
Kama tutaserereka katika msingi huu, basi ni bora Chambi ukafunga virago na kusitish huu mtandao. Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususa ni baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano. Sijui nyie wenzangu mmesimamia wapi katika suala hili.
Kama tutaserereka katika msingi huu, basi ni bora Chambi ukafunga virago na kusitish huu mtandao. Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususa ni baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano. Sijui nyie wenzangu mmesimamia wapi katika suala hili.
Naomba
niseme mwanzoni kabisa kwamba nchi yetu hii leo imefikia mahali ambapo
wasomi, wanazuoni kama sisi katika mtandao huu, Hatuna budi kujitokeza
na kuhesabika tunamuunga nani mkono katika uchaguzi ujao wa Rais wa
Tanzania. Tuwe wakweli na siyo kuendelea kuegemea katika kificho cha
'uhuru' wa wanazuoni katika kutoa maomi na fikra kama vile sisi si
wapiga kura au wananchi wanaothamini umuhimu kuhusu uongozi wa nchi
yetu. Wakati huo umepitwa na hali halisi ya itikadi na maana muhimu ya
uongozi wa Taifa.
Sasa,
Mimi binafsi, namuuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa. Yako mengi ambayo
kazuliwa huyu ndugu yetu; tunaambiwa tangu 1995 wakati Mwalimu Julius
Nyerere alipotamka kwamba 'huyu kijana ninalo faili lake, ana utajiri
usiyoelezeka. Ana nyumba kadhaa.' Lakini huyo huyo Baba wa Taifa
alimpenda sana Edward na kumpa madaraka ndani ya CCM na baraza la
mawaziri. Kama Edward alikuwa 'corrupt' swali ni kwanini Baba wa Taifa
hakumchukulia hatua za kisiasa na kisheria? Kwanini aseme hayo
aliyoyasema mwaka 1995 wakati Edward Lowassa alikuwa akiongoza kupendwa
dani ya CCM, ngazi zote na akitarajiwa ndiye angependekezwa kuwa mgombea
wa Urais? Jamani, wanazuoni, lazima mtafakari historia na hali halisi
ilivyokuwa. Mhe Jakaya Kikwete hakuwa 'the favourite' candidate in 1995.
Na Mwalimu alimtaka Ben Mkapa wakati ule awe Rais. Ilibidi Lowassa
atoswe kinamna!
Mimi
namfahamu Edward, Ninyi mnaujua huo utajiri wake au basi akitoa
michango hapa na pale ni pesa zake? Kati yenu mna utajiri zaidi ya
Edward. Edward alivumilia na kumsaidia mwenzake (nasita sasa hivi
kutumia neno 'rafiki') Jakaya ashinde uteuzi wa mgombea wa CCM hapo
2005. Aliamua hivyo baada ya makubaliano ya 1995. Wapo wengi wa Tanzania
waliyojitolea muhanda, wa hali na mali kuungana na Edward kumwezesha
Jakaya Kikwete kuwa Rais 2005. Kati yao, ndiyo wamekuwa karibu na Edward
katika kinyang'anyiro cha majuzi Dodoma. Imani yao ilikuwa kwamba
pamoja na mkanganyiko wa Februari 2008 wa Richmond ambao hauna mashiko
yoyote ya ufisadi kwa maana ya rushwa, Rais Kikwete angemfungulia mlango
mwenzake Edward kuwa mgombea wa CCM. Badala yake Edward bado akajengewa
mzengwe wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995. Hivi leo
tukichambua nani kati yetu ni tajiri zaidi ya Lowassa tutakuwa na
viongozi wanao kidhi mategemeo yetu?
Kuhusu
hili swala la Richmond: Hivi baada ya taarifa ya Tume ya Bunge ya Dr
Mwakyembe, Serikali ilitoa majibu. Mbona kwenye tuhuma za Bunge kuhusu
Tegeta Escrow imekuwapo taarifa toka kwa Chief Secretary kuhusu suala
hilo? Nani aliyejaribu kutoa maelezo ambayo yangemfungisha Lowassa au
kumkomboa kwa kitendo chake cha kujiuzuru kisiasa? Badala yake,
wanazuoni wenzangu ambao sidhani kama tunazo facts za kutosha
tunaendelea kumshutumu Lowassa na kumwona kama vile ni corrupt na
kiongozi asiyefaa. It is not fair.
Mimi
simlaumu Lowassa kujitoa CCM. Ni haki yake na kajieleza vipasavyo
kuhusu maamuzi yake. Je, ni uamuzi wa uroho kuhusu Urais? Jamani,
wanazuoni, hivi kweli tumefikia hatua ya kumwona mtu ana uroho wa Urais?
Ili awe au afanye nini ambacho sisi tufunge macho, na siyo tu kutoona,
bali pia kuto chukua hatua? Ikifikia hapo, basi hatuna Taifa tena!!
Taifa
letu limebahatika kufika hapa lilipofika mwaka huu. Wengi hatukutarajia
kwamba yale ambayo tumekuwa tukitafakari na hata kusali ghafla
yameibuka. Sidhani na siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu
itabaki ilivyo ifikapo Desemba 2015. Ni ishara ya kheri na mwelekeo
mwafaka kwa demokrasia ya Taifa letu.Naamini kwa dhati kabisa kwamba
Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye atasaidia ramani hii kuwba na
muono mpya.
Juma Volter Mwapachu

0 comments:
Post a Comment