Zarinah Hassan ‘Zari’ (mama Tiffah). Mwandishi wetu
KIMENUKA!
Baada ya madai kwamba mtoto Latifah ‘Tiffah’ si damu ya Mbongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku shemeji wa zamani wa Zarinah Hassan ‘Zari’
(mama Tiffah), King Lawrence naye kusema mtoto huyo ni wake, kuna
taarifa mpya zinazodai kuwa, Zari ameitwa kwao, Uganda ili akamalize
ubishi juu ya suala hilo, Risasi Jumamosi limenasa mchapo kamili.
Hivi karibuni baada ya Zari kujifungua, King Lawrence alijitokeza na
kudai kuwa, mtoto huyo ni wake na kusema kama kuna anayebisha kiitishwe
kipimo cha vinasaba (DNA), hivyo kuibua mkanganyiko na taarifa
zilizozagaa awali kuwa, mtoto huyo ni wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan
Ssemwanga.
0 comments:
Post a Comment