Monday, August 3, 2015





¤Hii picha ilipigwa Jumapili ya tarehe 26-Jul-2015 Bahari Beach Hotel ¤Ndio siku ya mwisho ambayo Dr Slaa alionekana kwenye vikao vya CHADEMA ¤Alitoa masharti ya jinsi ya kumpokea Lowassa, masharti ambayo yalipuuzwa.

 

¤Kesho yake (Jumatatu 27-Jul-2015) akaona press conference ambayo James Mbatia alipewa kazi ya kumkaribisha EL UKAWA
¤Alichofanya Dr Slaa ni kuandika barua ya kujiuzulu ukatibu mkuu. Baadaye akaandika barua ya kujivua uanachama wa CHADEMA. Siku nyingine akakabidhi gari alilokuwa analitumia kama katibu. Ijumaa iliyopita (31-Jul-2015) alikabidhi nyaraka zote za chama alizokuwa nazo.
 

¤Hivi sasa hakuna kiongozi hata mmoja wa CHADEMA mwenye uwezo wa kuwasiliana naye. Simu yake haipatikani.
¤Inasemekana ana mpango wa kuachana kabisa na siasa.
¤Moja ya maandalizi yaliyofanyika ni Tundu Lissu kusema yeye ndio aliandika "List of Shame" na Dr Slaa aliisoma tu. Mwaka 2007 Lissu hakuwa hata mbunge.
 

¤Mbowe anasema Dr Slaa amepewa likizo. Umewahi wapi kuona mwanajeshi anachukua likizo kipindi ambacho vita inakaribia kuanza? ¤Kimkakati, nafasi yake imetangazwa kuwa wazi labda hadi uchaguzi upite ili isiathiri matokeo ya uchaguzi.

0 comments:

Post a Comment