Tuesday, August 25, 2015

Mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Bw Frederick Mwakalebela kushoto akiwa ameongozana na katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Elisha Mwampashi 
Mwakalebela kushoto akimnadi amgombea udiwani wa kata ya Kwakilosa Bw Hamid Mbata

Na MatukiodaimaBlog
CHAMA cha wazee wilaya ya Iringa mjini kimesema kuwa kutona na mbunge aliyemaliza muda wake jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) jimbo hilo kwa sasa wanatamani kuona linarudi kwa mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Bw Frederick Mwakalebela .


Katibu wa chama hicho cha wazee wilaya ya Iringa mjini Edson Sanga alisema hayo katika viwanja wa CCM wilaya ya Iringa mjini kuwa jimbo hilo la Iringa mjini limeonekana kuwa nyuma kimaendeleo kutokana na mbunge aliyekuwepo kuendekeza marumbano zaidi na serikali na kushindwa kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi wake kama ilivyo kwa wabunge wengine wa CCM wanaomzunguka kama Isimani kwa Bw wiliam Lukuvi na jimbo la Kalenga kwa Godfrey Mgimwa .


Alisema kasi ya maendeleo katika majimbo jirani huwezi linganisha na jimbo la Iringa mjini ambalo maendeleo yanayoonekana ni yale aliyoacha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Bi Monica Mbega na kipindi cha miaka mitano ya Mchungaji Msigwa katika jimbo hilo zaidi ya maandamano na lugha za kejeli kwa wananchi hakuna kilichofanyika ,hivyo ni lazima wananchi wa jimbo la Iringa mjini kutorudia kosa kama la mwaka 2010


" Tunajua wana CCM ndio tuliompeleka bungeni mchungaji Msigwa baada ya chama ngazi ya juu kutosikiliza ma hitaji ya wananchi wa jimbo hilo hasa wana CCM ambao walimpitisha katika kura za maoni na vikao vya juu kukata jina lake ......ila kilichofanyika mwaka huu kwa kurejesha jina la mshindi huyo Bw Mwakalebela ni sawa na kurejesha ushindi kwa CCM"


Bw Sanga alisema yeye akiwa katibu wa chama cha wazee mwenyekiti wake alikuwa ni marehemu babake na Mwakalebela na kuwa siku zote wazee wa jimbo la Iringa walikuwa kama wapweke kutokana na mbunge huyo kuendeleza makundi na visasi .


Alisema moja kati ya ahadi ambayo mchungaji Msigwa alipata kuwaahidi wazee hao wakati wa kampeni ni pamoja na kutenga bajeti kupitia mfuko wa jimbo kwa ajili ya kuwasaidia wazee na yatima ila hadi leo hajapata kuonyesha hata senti moja iliyotengwa kwa ajili ya wazee hao jambo ambalo linawafanya kujutia kura zao walizompatia mwaka 2010.


Sanga alisema ilikuwa ni vema mbunge Msigwa angetembelea kujifunza kwa mbunge wa mwaka mmoja wa jimbo la Kalenga kijana Mgimwa ambae ndani ya mwaka mmoja alifanya mambo makubwa jimbo kwake tofauti na mbunge wa miaka mitano ambae hana jipya la kuonyesha kwa muda wote aliokuwepo madarakani .


Huku Bi Salome Kalinga mkazi wa Kihesa Kilolo akidai kuwa ushindi wa CCM unatokana na wana CCM wenyewe na ushindi wa Chadema kwa jimbo la Iringa mjini utaletwa na wana CCM iwapo wataendeleza makundi kama mwaka 2010 kwani kihalisia idadi ya wana CCM na wale wa vyama vya upinzani jimbo la Iringa mjini bado CCM wapo wengi zaidi ila makundi na visasi za kisiasa ndivyo vinavyopelekea chama kupoteza ushindi wake .


Katibu wa CCM kata ya Miyomboni Kitanzini Bw Rayson Shayo alisema kuwa kata yake ambayo ndio kata iliyopo katikati ya mji wa Iringa hadi sasa wanajutia kumchagua Msigwa kutokana na vurugu za mara kwa mara ambazo chimbuko lake ni mbunge huyo ikiwemo vurugu ya machinga kuruhusiwa na mbunge huyo kufanya kazi katikati ya barabara.
NA MATUKIO DAIMA

0 comments:

Post a Comment