Tuesday, August 11, 2015

  • ¤Moja ya manufaa na faida kubwa ya Lowassa kuhamia UKAWA ni upinzani kujua siri za CCM, kujua mbinu, nguvu na udhaifu wa adui kama kwenye sana ya vita (The Art of War)

    ¤Hii ni kama mwaka 2002 Raila Odinga alipojiondoa KANU na kujiunga na UKAWA ya Kenya (Coalition ya NARC). Kibaki alikuwa kiongozi wa DP huku Raila akianzisha LDP.


    ¤Tofauti ya Raila na Lowassa ni kwamba Raila hakugombea urais. Raila alimsaidia Mwai kushinda uchaguzi wakati Lowassa yeye ndio mgombea urais. Kwenye kampeni ya Kenya, Raila alikuwa anasema "KIBAKI TOSHA".

    ¤Nilitegemea Lowassa angetumika kumsaidia Dr Slaa kushinda. Haikuwa hivyo.

    ¤Lowassa alienda Buguruni Makao Makuu ya CUF kuhutubia wanachama wa CUF baada ya Lipumba kujiondoa uenyekiti. Akasema CCM ni mabingwa wa kuiba kura.
    ¤Huyu ndio alikuwa mwenyekiti wa timu ya kampeni iliyomuingiza JK madarakani mwaka 2005.

    ¤Najiuliza ni lini ameanza kujua kwamba CCM ni mabingwa wa kuiba kura. Amejua baada au kabla ya kuondoka CCM? Ni kwa nini hajawahi kusema hivyo kabla? Angeendelea kubaki CCM angesema hayo? Je hasingekatwa angeendelea kubaki na hiyo siri? Kwa nini alitumia nguvu nyingi sana kutaka kugombea urais kwa chama kinachoiba kura?

    ¤Je, akishinda uchaguzi, hawezi na yeye kuzitumia mbinu hizo (election rigging) alizozinyamazia kimya kwa muda mrefu ili asiondolewe madarakani kwenye chaguzi zinazofuatia chama chake kikiwa kimeshika dola?

  • Mohamed Ayub Mzilla Kiongozi naona safari umeamua kumuelezea lowassa,kuna nani hapo kiongozi au kuna ka post upande wa pili?
    Like · Reply · 1 hr
  • CM Mgaza Una mawazo mazuri sana, ila soma alama za nyakati kizazi hiki wanataka mabadiliko kwa hiyo ccm watake wasitake lazima watoke ktk madaraka mfano halisi ni tukio la jana, mbona jibu liko wazi?
    Like · Reply · 1 hr
  • Seleman Matipa Kuna mambo mengi sana yatatokea baada ya uchaguzi bila kujali matokeo yatakuwaje.
    Like · Reply · 1 hr
  • CM Mgaza Ni kweli na amani yetu iko mashakani kama matokeo yatachakachuliwa
    Like · Reply · 1 hr
  • Sebastian Liduke Kaka William Kaijage ndo maana competition huwa inakuwa na kaumuhimu wake kwa wananchi , nafikiri tulipofikia kwamba hakuna chama ambacho kinajiona kinammiliki nchi ni hatua nzuri kwa wananchi , kwasababu itamfanya yeyote anayechaguliwa kuwa makini ,
    Like · Reply · 1 hr · Edited
  • Sebastian Liduke Power tends to corrupt and absolute power corrupts absolutely.
    Lord Acton
    Like · Reply · 1 hr
  • Respicius Francis kumbe kibaki na odinga walikuwa marafik??
  • William Kaijage DIBWE
    Napenda kumzungumzia Lowassa maana ndio mgombea maarufu kuliko wote mwaka huu.
  • Elineema Kisanga lowasa asingeweza kusema lolote baya la ccm akiwa ndani ya ccm sasa kashatoka nje ya ccm Anahaki ya kusema yoote maana hayupo tena ndani ya mfumo wa ccm Ameelewa sasa ndiyo maana anataka mabadiliko kama alishiriki kuiba kura sasa hataki tena anataka mabadiliko (mf mtu akifanya dhambi kisha akagundua dhambi yake Akaitubia Anasamehewa Amegeuka sasa Tusiikumbuke tena dhambi ya huyu mtu ameshaitumbia?

0 comments:

Post a Comment