Thursday, August 13, 2015

Mwanamitindo wa Venezuela, Jeinny Lizarazo ameendelea kugonga vichwa vya habari barani Ulaya.
Mapema wiki hii alidai kwamba Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa nyota wa Real Madrid, Karim Benzema, lakini mpaka sasa haijatokea.
Lizarazo alifafanua kwamba Benzema anaelekea kuchukua vipimo vya afya Emirates.
Leo mrembo huyo amewapoza mashabik wa Arsenal akisisitiza kwamba lazima dili hilo litokee, huku akifika mbali zaidi kwa kusema kwamba, kama taarifa yake sio sahihi mpaka Agosti 29 mwaka huu, yuko tayari kupata adhabu yoyote ile.
Tunza tarehe hii kwenye kitabu chako...manake kakubali adhabu yoyote unayoona safi.....

0 comments:

Post a Comment