STAA
mdogo kwenye kiwanda cha filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’
ameonekana kumrushia vijembe hasimu wake mkubwa mlimbwende Husna Maulid
kwa kile alichodai kuwa anamuibia maelezo yake ya picha (caption) kwenye
mtandao wake wa Instagram.
Staa huyo ambaye hakumtaja Husna moja kwa
moja, alisema kwa sababu amekuwa akiweka maelezo ya picha
katika
mtandao na mtu kuyaiba kama yalivyo na kuweka katika picha zake, ameamua
kutoa onyo ili asiibiwe.
“Naweka caption lakini ina hati miliki,
wewe unayechukua na kuhamishia kwako, tafadhali.” Aliandika Lulu
mtandaoni ambapo alipoulizwa na mwandishi wetu kama alimtupia vijembe
Husna, alisema:
“Jamani sijataja jina la mtu yoyote lakini kama kuna ambaye anajihisi basi ndio huyohuyo.”
Husna
amekuwa akikopi maneno ambayo Lulu anayaweka katika kurasa zake kama:
“You can copy my things but you can’t be me.” Husna naye anaandika
hivyohivyo.
Wawili hao waliwahi kuwa marafiki kisha kutofautiana wakituhumiana kuibiana bwana.
0 comments:
Post a Comment