Posted by Williammalecela.com on Thursday, August 20, 2015
 |
| UKAWA na Safari ya Matumaini kwa Waganga wa Kienyeji live!! |
 |
Mabasi mapya ya kwanza East Africa nzima kuletwa na Serikali ya CCM Awamu ya Nne na kuanza majaribio majuzi Dar live!!
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA DART.
Kuna upotoshaji wa Makusudi uliozagaa kwenye Mitandao ya Kijamii kuwa Mabasi Yaliyozinduliwa Tarehe 17/08/2015 kuwa.
1. Mabasi niya Kichina
2. Milango ya kushukia na kupandia Abiria Iko kushoto hivyo hayaendani na Miundombinu iliyojengwa.
HUO NI UZUSHI WENYE LENGO LA KUWAPOTOSHA WATANZANI WALIOCHOSHWA NA MSONGAMANO UNAOONGEZEKA SIKU HADI SIKU
TAARIFA SAHIHI KUTOKA KWENYE MAMLAKA HUSIKA HII HAPA:
1. Kiwanda Kilicho Assemble (Kuunganisha) Mabasi haya kinaitwa Golden Dragon cha China.
2. Aina ya Injini ni CUMMINS ya Marekani (USA)
3. Aina ya Giaboksi ni VOITH ya Ujerumani.
4. Mfumo wa Stelingi ni ZF ya Ujerumani.
5. Mgumo wa Difu ni kutoka Marekani (USA).
6. Aina ya Suspension (Za upepo) Air Suspension kutoka Marekani (USA).
7. Mfumo wa Breki ni WABCO
8. Aina za Mabasi ziko mbili. Articulated Mita kumi na nane almaarufu
(Ikarusi) Kutoka Hungary zitakazopita kwenye barabara Maalumu za zege
zilizojengwa na Mabaai ya mita kumi na mbili yanayoitwa (Feeder) Mabasi
Mlisho yatakayotumia vituo vilivyoko nje ya mfumo Mfano Kituo cha
Shekilango, Moroco Hotel, Mwanamboka na Magomeni Mapipa kuwapeleka na
kuwaleta kwenye Mfumo.
9. Milango ya kupanda na kushukia Abiria
ipo kulia na kushoto ili kukidhi mahitaji ndani na nje ya mfumo ambayo
idadi yake ni Minne kila upande ila itatumika mitatu na mmoja niwa
dharula kila upande.
10. Urefu kutoka ardhini kwa milango ya
kushoto ya Basi ni Sentimita thelathini (30) ambayo hata mtoto anaweza
kushuka bila msaada wa mtu mzima.
11. Urefu wa Milango ya kulia
ni Sentimita tisini (90) sawa na urefu wa Platform za kila kituo cha
DART unaomuwezesha hata mtu mwenye mahitaji maalum Kuingia na kutoka
ndani ya basi bila msaada wa mtu.
12. Ndani ya basi kuna eneo la kukaa watu wenye Mahitaji maalum. Walemavu, Wazee na Mama wajawazito.
13. Mfumo wa ulipaji nauli unafanyika vituoni kama ilivyo kwenye kivuko
pale Kivukoni hivyo basi hili halina Kondokta. Makondakta wapo vituoni.
14. Muda wa Safari kutoka Kivukoni hadi kimara ni wastani wa dakika
thelathini (30) ikihusisha muda wa kushusha na kupakia kwenye Vituo vya
DART.
15. Ni marufuku kwa chombo ama mwananchi kutumia barabara
maalum za Mabasi. Wananchi watumie maeneo yaliyotengwa maalum kulingana
na mahitaji. Watumiaji wa Bodaboda wanatakiwa kupita kwenye barabara
zinazotumiwa na magari ya Kawaida na siyo eneo lililotengwa kwa ajili ya
Watembea kwa Miguu.
KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISI ZA WAKALA WA MABASI JENGO LA UBUNGO PLAZA GHOROFA YA KWANZA
|
0 comments:
Post a Comment