Thursday, August 27, 2015







UKAWA HUENDA WAMESHINDWA KABLA HATA HAWAJAANZA …27/8/2015


Kama ingekuwa ni mechi ya mpira wa mguu, UKAWA ingefananishwa na timu ambayo kocha dakika za mwisho ameshindwa kuja uwanjani kutokana na matatizo ya kifamilia. Pia wachezaji wawili wanaotegemewa sana wametolewa kwa kadi nyekundu. Hivyo timu haina mwongozo na pia ina wachezaji pungufu huku morali ikiwa ya chini kabisa.

Mwisho wa kurudisha fomu za kugombea urais na ubunge ilikuwa ni Ijumaa (21-Aug-2015) na kampeni rasmi zimeanza Jumamosi tarehe 22-Aug-2015 .

Lakini mpaka sasa kuna dalili 5 kuu zinazoonyesha UKAWA itashindwa vibaya kwenye kura za urais na ubunge

1. TIMU YA KAMPENI

Timu ya kampeni ya UKAWA iliwahitaji sana Dr Wilbroad Slaa (Katibu Mkuu wa CHADEMA) na Prof Ibrahim Lipumba wa CUF.

Dr Slaa alihitajika zaidi kwa vile Lowassa ana kazi mbili kubwa kwenye kampeni. Kwanza ni kujisafisha kwa kashfa za ufisadi na pili kuelezea nini atafanya ambacho ameshindwa kukifanya kwa miaka mingi aliyokuwa serikalini katika vyeo tofauti ikiwemo uwaziri mkuu kwamba ni lazima apewe urais.

Kwenye suala la kujisafisha, Dr Slaa ndiye aliyekuwa akihitajika zaidi kumsaidia maana Dr Slaa ndiye aliyekuwa mbeba hoja mkuu ya kuwapinga mafisadi akiwemo Lowassa aliyemtaja katika “List of Shame” Jumamosi ya tarehe 15-Sep-2007 katika viwanja vya Mwembeyanga.

Hawa wawili (Dr Slaa na Prof Lipumba) wamejitoa kwenye timu wote hawapo kwenye timu. Hii imeleta picha ya UKAWA kutokuwa wamoja na kuwakilisha kundi kubwa la wanachama ambao hawaafiki Lowassa kujiunga na UKAWA na kupewa ugombea urais.

Makada wakuu wengine wa UKAWA wote watakuwa majimboni kunusuru ubunge. Freeman Mbowe atakuwa jimboni Hai. Tundu Lissu atakuwa jimboni Singida Mashariki. James Mbatia atakuwa Vunjo. Emmanuel Makaidi atakuwa Masasi. Godbless Lema atakuwa Arusha Mjini. John Mnyika atakuwa Kibamba. Lowassa ataachwa na mkiwa.

2. KUSAMBARATIKA KWA MAAFIKIANO

Umoja wa UKAWA mkoa wa Mara wilaya ya Serengeti umesambaratika na kila chama (kati ya vyama vi-4) kimesimamisha mgombea wa ubunge na udiwani kwenye kila kata.

Jimboni Segerea wana UKAWA watatu wamewakilisha fomu za kugombea ubunge. Waliowakilisha ni wagombea wawili wa CHADEMA sambamba na Julius Mtatiro wa CUF.

Taarifa zinaonyesha, kuna majimbo kama 20 ambayo zaidi mgombea mmoja wa UKAWA amewakilisha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi.

3. WABUNGE WA CCM KUSHINDA BILA KUPINGWA

Pia kuna majimbo kadhaa ambayo wabunge wa CCM wamepita bila kupingwa kutokana wagombea kutowarejesha fomu za ugombea ubunge kwa msimamizi wa uchaguzi au kutokana na kushindwa kwenye mapingamizi.

Mpaka sasa kuna majimbo ma-4 ambayo CCM wameshinda bila kupingwa. Majimbo hayo ni Bumbuli, Ludewa, Nanyamba na Mlalo.

4. MAANDAMANO YA KUPINGA WAGOMBEA WALIOPITISHWA

Maeneo mengi kumekuwa na malalamiko na maandamano kupinga walioteuliwa kugombea ubunge kwa upendeleo wa uongozi wa juu wakati walishindwa kwenye kura za maoni.

Baadhi ya maeneo hayo ni jimbo la Bunda amesimamishwa Ester Bulaya ambaye alishindwa kwenye kura za maoni.

Jimboni Kishapu, watu wamepinga uteuzi wa Fred Mpendazoe kuwa mgombea ubunge.

Hii ni bila kusahau jimboni Ukonga ambako Mwita Witara ameteuliwa kugombea ubunge wakati alishindwa kwenye kura za maoni kwa vile tu ana ukaribu na Freeman Mbowe.

5. UZINDUZI WA KAMPENI WABUMA

Uzinduzi wa kampeni ilikuwa ufanyike Jumamosi tarehe 22-Aug-2015

Uzinduzi wa kampeni ukashindwa kufanyika kwa kisingizio cha kunyimwa uwanja wa Taifa

Lakini habari za ndani zinasema uzinduzi ulishindwa kufanyika kutokana na hali tata na tete ya kiafya ya mgombea urais

Pia hadi kufikia siku hiyo, ilani ya uchaguzi ya UKAWA ilikuwa haijaeleweka.

Badala yake wakaahirisha uzinduzi hadi tarehe 29-Aug-2015 ili waweze kujifunza kutoka kwa CCM.

Kampeni ya siku 63 sasa itakuwa siku 56. Mabadiliko mabovu kama haya yanatia wasiwasi kama wana hata ratiba inayoaminika ya mikutano ya kampeni ya nchi nzima.

THE KING OF ALL BONGO SOCIAL MEDIA NETWORK!!

Le Mutuz Nation

0 comments:

Post a Comment