Sunday, August 30, 2015

Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini leo kimezindua rasmi kampeni zake za Uchaguzi mkuu ujao katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga,ambapo wabunge wa majimbo yote ya Shinyanga wamehudhuria uzinduzi huo .Uzinduzi huo umeongozwa na waziri wa Uchukuzi mheshimiwa Samweli Sitta na mbunge wa Mtella aliyemaliza muda wake Livingstone Lusinde ambao walitumia fursa hiyo kumnadi mgombea urais wa CCM Dkt John Magufuli na kumponda mheshimiwa Edward Lowassa wakidai kuwa hafai kuwa rais kutokana ufisadi wake na kwamba Ukawa wamekurupuka kwani hawamjui vizuri Lowassa.Makada hao wa CCM pia walisema Lowassa hana lolote zaidi ya mbwembwe na visingizio vya hapa na pale-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Wanachama wa CCM na wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa CCM katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga leo



Makada wa CCM wakiwa eneo la tukio


Mjumbe wa NEC taifa Gasper Kileo akizungumza katika mkutano huo ambazo aliwataka wanaccm kuwapuuza watu wanaozusha kuwa atahamia Chadema/Ukawa kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni rafiki yake na Lowassa,ambapo Kileo alisisitiza kuwa hajawahi na wala hafikiria kuhama CCM na kwamba CCM lazima ishinde katika uchaguzi mkuu ujao


Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CCM wilaya ya Shinyanga mjini


Mheshimiwa Samweli Sitta akizungumza katika mkutano huo,ambapo aliwatambulisha wagombea ubunge majimbo yote 6 ya uchaguzi mkoa wa Shinyanga ambayo ni Ushetu,Msalala,Kahama mjini,Kishapu,Shinyanga mjini,Kishapu na Solwa na kusisitiza kuwa lazima CCM ishinde katika majimbo hayo.


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal akiwasalimia wakazi wa Shinyanga na kuwaomba wananchi kuchagua wagombea wa CCM kwani ndiyo watawaletea maendeleo


Wanachama wa CCM wakifuatilia kilichokuwa kinajiri uwanjani


Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wananchi kuwapa kura wagombea wa CCM


Mgombea ubunge jimbo la Msalala mheshimiwa Ezekiel Maige akiwasalimia wakazi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga




Mgombea ubunge jimbo jipya la Ushetu mheshimiwa Elius Kwandikwa akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo ajigamba kuwa katika jimbo lake wameshamaliza kufanya uchaguzi wanachosubiri ni utaratibu tu tarehe 25 Oktoba mwaka huu.


Mgombea ubunge wa jimbo la Kishapu mheshimiwa Suleiman Nchambi akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wanaShinyanga kuwapa kura wagombea wa CCM kwani ndiyo watakaowaletea maendeleo watanzania


Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wakazi wa Shinyanga kutochagua mbunge ambaye siyo mzawa wa Shinyanga na badala yake wampe yeye kura ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Shinyanga huku akijisifu kuwa amefanya mambo mengi ya kimaendeleo kwa wananchi katika sekta mbalimbali kama vile afya,elimu,michezo n.k


Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wakazi wa Shinyanga leo


Mheshimiwa Samweli Sitta akiwahutubia wakazi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini ambapo alisisitiza kuwa mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa anahusika na sakata la Richmond na utajiri wake haueleweki




Msanii wa nyimbo za asili Madebe Jinasa akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini


Wafuasi wa CCM na wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa CCM leo mjini Shinyanga


Mkutano unaendelea


Mkutano unaendelea


Mheshimiwa Livingstone Lusinde akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alitumia muda mwingi kumponda mgombea urais kupitia Ukawa Edward Lowassa hasa kuhusu afya yake kwamba ni mgonjwa bila kutaja ugonjwa anaougua/anaoumwa


Wanachama wa CCM wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kwenye mkutano


Mheshimiwa Livingstone Lusinde akizungumza mjini Shinyanga 


Wafuasi wa CCM wakiwa eneo la tukio


Mheshimiwa Lusinde akiwaombea kura wagombea wa CCM na kumpa sifa kem kem mheshimiwa John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM 


Mkutano unaendelea


Mkutano unaendelea




Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano wa CCM leo


Mkutano unaendelea




Mkutano unaendelea




Wananchi wakifurahia jambo kwenye mkutano


Mkutano unaendelea




Mheshimiwa Lusinde akiwahutubia wakazi wa Shinyanga




Tunafuatilia kinachoendelea hapa.....


Mheshimiwa Lusinde akiwa na wagombea ubunge majimbo yote ya Shinyanga,ambapo mmoja pekee wa jimbo la Solwa mheshimiwa Ahmed Salum hakuwepo kwenye mkutano huo kutokana na kuwa katika shughuli zingine za kichama




Wabunge watarajiwa majimbo ya Shinyanga wakiwa jukwaani




Wa tatu kutoka kushoto ni mgombea ubunge jimbo la Kahama mjini mheshimiwa Jumanne Kishimba




Wanachama wa CCM wakicheza uwanjani


Baada ya mkutano kila mmoja akaendelea na shughuli zake wengine wakapanda kwenye magari yao kurudi makwao




Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano




Wazee wa CCM wakiwa eneo la tukio


Vijana wa Greenguard wakiwa eneo la tukio


Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

0 comments:

Post a Comment