Sunday, August 16, 2015

WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiaga kuashiria kumaliza uongozi wake wa miaka kumi, huku kampeni za kumpata mrithi wake zikikaribia, wazee wastaafu waliofanya kazi na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wamezungumzia historia ya uongozi wa nchi yetu, huku marais wastaafu waliomfuatia, wakieleza changamoto walizokabiliana nazo katika miaka kumi ya kila mmoja wao. 
Mbali na wastaafu hao, Rais Kikwete ambaye jana alikiri kuwa yuko karibuni kuanza kuitwa mzee, naye amezungumzia namna alivyokabiliana na changamoto za uongozi wake, huku akizungumzia anachojutia katika miaka kumi ya uongozi wake. Haya yamo kwenye Ripoti ya Benki ya Dunia ambayo inaelezea kwa mara ya kwanza kufanikiwa kwa uchumi wa Tanzania na changamoto zake ikiwemo kuyumba kwake kwa zaidi ya miaka 50, tangu wakati wa Uhuru mwaka 1961 mpaka mwaka huu na kutoa jibu la kukua, kuanguka na kuibuka kwa uchumi wa viwanda Tanzania. 
Mafanikio ya Mwalimu Katika ripoti ya kihistoria ya miaka 50 ya ushirikiano wa Tanzania na Benki ya Dunia iliyotolewa hivi karibuni, washauri wa mwanzo wa Mwalimu Nyerere na watendaji wa sekta muhimu akiwemo Profesa Simon Mbilinyi na Ibrahimu Kaduma, wamekaririwa wakizungumzia uongozi wa Mwalimu Nyerere ulivyokuwa. Ripoti hiyo inaweka bayana kuwa Mwalimu Nyerere aliongoza nchi iliyokuwa katika mfumo wa Kijamaa, ambao ulisimamia Serikali kuwa mpangaji na msimamizi mkuu wa shughuli za kiuchumi.

0 comments:

Post a Comment