KABAANG!
Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ amenaswa
kimalovee na rafiki wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku
ikidaiwa ni ‘mtu’ wake.
Chanzo
makini kililiambia gazeti hili kwamba jamaa huyo ambaye anajiita
Dangote Kifyagio ni rafiki wa Diamond ambaye alikuwa akimsaidia mambo
yake kimuziki ili awe juu.
“Ndiyo
maana kuna picha kibao ambazo zinawaonesha wakiwa romantic kiasi kwamba
wapo wanaokwenda mbali na kusema ni wapenzi, watu bwana,” kilidai
chanzo hicho na kuongeza:
“Unajua
yule Kifyagio alikuwa rafiki wa Diomond sana huko nyuma, sasa isije
ikawa kaamua kujiweka kwa shemeji yake maana si unawajua tena hawa
mastaa wetu, nyie fuatilieni mtaujua ukweli.”
Baada
ya gazeti hili kunasa ‘ubuyu’ huo pamoja na picha za Wema na jamaa huyo
wakiwa kimahaba sehemu tofautitofauti, lilimvutia waya mrembo huyo na
kumbana kuhusu uhusiano =wake na Dangote Kifyagio ambapo simu yake
haikupokelewa.
Alipotumiwa ujumbe juu ya madai kuwa anatembea na jamaa huyo alijibu kwa hasira kama ifuatavyo:
“Halafu
sikia nikwambie, vitu vingine ni upuuzi tu hivyo vitu vinaniharibia
deal zangu na mipango yangu yote, sipendi hata kidogo, yaani sipendi
kwanza kufuatiliwa, amekuwa mtu wangu? Nishawahi kumposti na kusema ni
bwana’angu zaidi ya mimi na yeye kuheshimiana? Nina bwana wangu ambaye
ndiye kila kitu kwangu jamani sipendi wallah…sipendi.”
0 comments:
Post a Comment