Posted by Williammalecela.com on Wednesday, September 23, 2015
 |
Mkuu Mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Amos Makalla, amefanya operesheni ya kushitukiza ya
kufyeka na kungoa mirungi zaidi ya ekari 10 katika kijiji cha Rindini,
kata ya Gavaosaweni wilaya ya same.operesheni imehusisha Kamati ya
Ulinzi mkoa n wilaya, watendaji wa serikali na askari wanafunzi 100 wa
Chuo cha polisi Moshi. Vijiji 28 na kata 13 wilaya ya Same wananchi wamelima mirungi ekari 260
Ametoa wiki 2 kwa wananchi wote waliolima mirungi kufyeka na kuiongoa
kabisa na mwananchi yeyote atakayekataa kutekeleza ameagiza kufanyika
operesheni kabambe ya kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria
Mirungi kwa mujibu wa sheria ni miongoni mwa madawa ya kulevya na
ukipatikana na hatia utahukumiwa kifungo si chini ya miaka 30. Jana
alijulishwa na wadau wa Elimu kuwa baadhi ya Shule katika wilaya ya same
zimekithiri kwa utoro na Matokeo mabaya kutokana na wanafunzi
kujihusisha na biashara ya Mirungi. |
0 comments:
Post a Comment