Viongozi watatu wa Chadema wilaya ya Kilosa na mwanachama mmoja
wametangaza kujiunga rasmi na CCM baada ya kuchoshwa na siasa za Chadema
ambazo wameona hazina haki.
Viongozi hao waliohamia CCM ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya
ya Kilosa Ndugu Selemani Simba, Katibu wa Chadema wilaya hiyo Ndugu
Ibrahim Abdallah Selemani, aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Kilosa Kati
Mussa Ngongo na aliyejitambulisha kama mwanachama kiherehere wa Chadema
Bi.Oliver Mollel.
Viongozi hao walitangaza kukihama chama cha Chadema kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni za CCM mbele ya mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John
Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Kilosa town.

0 comments:
Post a Comment