 |
| Mh. Davis Mosha akizungumza na wakazi wa kata ya Kiborilon |
 |
| Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Mh. Agrey Mareale akizungumza na Wananchi wa Kiboriloni |
Pia Mgombea huyo alizungumzia malalamiko ya Mzee Ndesamburo anayomtuhumu kumny'ang'anya wafanyakazi wake wawili ambao ni John Maarufu kama Laperee na mwingine aliyefahamika kwa jina Moja tu la Gaga. Mosha alisema ndesamburo anajua fika kwanini hawa vijana wapo kwangu na wananifanyia kampeni sasa kwanini leo apande jukwaani na kuwakana wakati tayari kuna makubaliano. Davis alikata mzizi wa fitina na kuwaita Jukwaani Gaga na Laperee na kuwapa nfasi wazungumze kwanini wapo na Davis na sio Jafari.
 |
| Mamia ya wananchi wa kiboriloni wakimsikiliza Mh. Davis Mosh |
Akiongea na Umati mkubwa wa Wananchi wa Kiboriloni Gaga alionesha ujumbe wa maneno katika simu yake ambao ulisomwa na mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano huo ujumbe ambao ulikua ukimuita Gaga aonane na Ndesamburo na ujumbe huo ulitoka kwa Ndesamburo. Gaga alisema yeye alitii wito wa bosi wake na kufika kwa Ndesamburo na akamkuta Davis Mosha na Ndesamburo baada ya Muda akaingia Laperee na kuanza Mazungumzo. Gaga alizidi kuongea akisema Mzee aliwatambulisha kwa Davis na kuwapa kazi ya kuhakikisha wanamnadi Davis mpaka anashinda ubunge na hawezi kuachia jimbo likaenda kwa mtu Chasaka (Akimaanisha Kabil tofauti na lake) na kuwaahidi kuwa yeye atakua nyuma yao na hatoweza kujionesha kwa kuwa ni kiongozi katika chama. Hivyo basi yeye na John wanafanya kazi maalumu ambayo wamepewa na Ndesamburo wananchi wasiwaone ni wasaliti wao wanatimiza kazi ya Bosi wao.
Laperee nae alipata fursa ya kuzungumza alisema yeye hawezi mtukana wala kumsema vibaya Mzee Ndesamburo, Anamuheshimu na yupo ccm kwa kazi maalumu ya kuhakikisha Davis anashinda kama walivyokubaliana na anachoweza kumuahidi ni kuwa ile ahadi yake ya pale kwenye kikao ataitimiza kwa asilimia miamoja na hatomuangusha.
0 comments:
Post a Comment