Mtoto aitwaye Chacha Robert, ugonjwa wa kuota magamba kwenye ngozi.
MATESO! Mtoto aitwaye Chacha Robert (15), (pichani), mkazi wa Musoma, Mara anateseka na ugonjwa wa ajabu wa kuota magamba kama ya nyoka sehemu ya mwili hali inayomsababishia kutengwa na jamii.
Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na familia yake zinaeleza kuwa, Chacha alizaliwa hivyo na mama yake mzazi alifariki dunia saa chache baada ya kujifungua.
“Wao kama Wakurya waliamini kwamba mama yake aliona chatu wakati akiwa mjamzito ndiyo maana mtoto akazaliwa hivyo.
“Chacha kwa sasa anasoma kidato cha kwanza kwa shida. Wanafunzi wenzake wanamnyanyapaa na kumuoneshea vidole kila anapopita,” alisema mtu huyo ambaye ndiye mwangalizi wa karibu wa maisha ya Chacha.
Akaendelea: “Tulimpeleka hospitali, daktari akasema ugonjwa huo unaitwa Ichthyosis ambao unafanana na Albinism anavyozaliwa. Na msaada anaouhitaji ni kubadilisha nguo mara kwa mara na kula vyakula vya kiasili.
“Kwa sasa, Chacha anaishi na baba yake na babu yake na hali yao kiuchumi si nzuri na ndiyo maana tumewaomba nyie Global mtusaidie.”
Picha kwa hisani ya Flora Show
0 comments:
Post a Comment