Kiongozi wa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya
Ngoma Africa band, Kamanda Ras Makunja amefunguka kwa kusema kuwa
yeye na kikosi kazi chake wanazo sababu zote za kumkubali mgombea urais wa chama tawala Mheshimiwa John Pombe Magufuli ashinde kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi mkuu utakao fanyika 25 oktoba 2015.Mkuu huyo wa Ngoma Africa band akikaririwa bila kigugumizi ameweka wazi kuwa John Magufuli anatufaa kuwa Rais wa nchi yetu na tunazo sababu zote za kumkubali,mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja amewaomba watanzania wote bila kujali itikadi na ushabiki wa vyama vyao wapigie kura za NDIO John Pombe Magufuli na Bi.Samia Suluhu Hassan. Mwanamuziki huyo aliweka wazi kuwa Tanzania tunahitaji
Rais mchapa kazi,Mkweli,mwenye umri ambao sio kijana mno wala sio mzee,rais mwenye maadili,kueshimu sheria na katiba ya nchi ,tunahitaji Rais anayeyajua machungu na kero za watanzania pia awe ameshapitia maisha ya kawaida ya mtanzania ,si mwingine bali John Pombe Magufuli

0 comments:
Post a Comment