Zikiwa zimebaki takribani siku 39 kuelekea siku ya Kupiga kura. Wasanii
wawili wa tasnia ya Maigizo waliokuwa katika Kampeni za Mh Edward
Lowassa wa CHADEMA ghafla wameamia kwenye Kampeni za Mh John P. Magufuli
wa CCM.

Hii imethibitishwa na mmoja wa wasanii hao, yaani Anti Ezekiel kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter. ( Auntezeofficial)

Ni stori ya kisiasa ambayo ilianza kuchukua headlines kwenye mitandao
mbalimbali kuhusu wasanii wawili wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Vicent
Kigosi aka Ray kuondoka UKAWA na kuhamia chama cha Mapinduzi.
Baada ya taarifa hizo kuchukua nafasi kubwa kwenye mitandao sasa ripota
wa millardayo.com amezungumza na Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa
kampeni ya Mama ongea na Mwanao…’Ndugu zetu wakina Vicent Kigosi na Aunt
Ezekiel walitoroka wamerudi CCM kabla hawajatangaza lakini watatangaza
wamerudi kwa kishindo kikubwa wanaamini bila hapo walipofika bila nguvu
ya Mh Jakaya Mrisho Kikwete wasingiweza kufika‘ – Steve Nyerere
.
‘Kwa hiyo nataka kuwaambia watanzania kuwa hao watu wamerudi katika
chama cha mapinduzi na wala msidanganywe pilika pilika za huku na kule
hawa watu ni wanachama wa CCM hai walitoroka na sifa ya kutoroka ni
kukosa nidhani kwa sisi wazazi ambao tuna watoto , mtoto akitoroka
unatakiwa umpe adhabu ili siku nyingi afahamu njia ya sahihi na njia
sahihi ni chama cha Mapinduzi ambacho kina Dkt John Pombe Magufuli na
Mama Samia Suluhu’ – Steve Nyerere
0 comments:
Post a Comment