Posted by Williammalecela.com on Thursday, September 17, 2015
 |
Lowassa: Nipeni bakora niwatandike mafisadi.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amefunguka na
kuwaomba Watanzania kumpa kura ambazo ameziita bakora ili awacharaze
viboko watu wote wanaojihusisha na vitendo vya ufisadi nchini.
Lowassa ambaye anaungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akihutubia umati
katika mkutano wa kampeni kwenye Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege,
mjini Morogoro.
Alisema ili kutekeleza azima yake, ni vizuri
wananchi wakajitokeza kwa wingi kama Oktoba 25, mwaka huu kama
walivyojitokeza jana wapige kura ili kumpa kazi ya kuwanyoosha mafisadi.
Akizungumza huku akikatizwa kutokana na kushangiliwa na umati, Lowassa
alisema Serikali yake itahakikisha inawashughulikia wale wote
watakaotumia vibaya fedha au madaraka waliopewa kinyume cha sheria na
taratibu.
Lowassa alijiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu mwaka 2008,
kama njia ya kuwajibika baada ya kuibuka kwa sakata ya serikali kuipa
zabuni kampuni ya kufua umeme ya Richmond katika mazingira tata.
Sakata hilo liliibuliwa na Kamati Teule iliyoongozwa na Mbunge wa kyela,
Dk. Harrison Mwakyembe, baada ya kuchunguza na kuwasilisha ripoti
bungeni
Source: Nipashe
|


0 comments:
Post a Comment