
Waziri
Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, amesema kama Lowassa atafanikiwa
kuingia madarakani Watanzania walioficha fedha nje ya nchi
watazirudisha.Sumaye alitoa kauli hiyo jana alipohutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Laini Polisi mjini Nzega, Mkoa wa Tabora.
Kwa
mujibu wa Sumaye, fedha hizo ambazo Serikali ya CCM imeshindwa
kuzirudisha zitatakiwa kurudi kwa sababu ni mali ya Watanzania.
“Jana
(juzi) mmemsikia Magufuli (Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli),
akisema atakapoingia madarakani atarudisha mashamba ya wananchi
yaliyoporwa.
“Kwanza
kabisa namwambia Magufuli kwamba Ikulu haingii, lakini sisi
tutakapoingia madarakani tutahakikisha walioiba fedha za Watanzania na
kuzificha huko Ulaya au Uswisi wanazirudisha,” alisema Sumaye.
Sumaye
pia alizungumzia suala la rushwa nchini na kusema kama CCM wangekuwa
waungwana wasingemsimamisha mtu yeyote kugombea urais kwa sababu
wameshindwa kuwaletea maisha bora Watanzania.
“Magufuli
anasema akiingia madarakani atakomesha rushwa sasa kama ana uwezo huo
kwa nini ameshindwa kuikomesha wakati na yeye ni waziri katika Serikali
iliyokithiri kwa rushwa?
“Magufuli
anasema akiingia madarakani atakuza uchumi, kama kweli ana uwezo wa
kukuza uchumi kwa nini ameshindwa kuukuza kupitia Serikali ya CCM ambayo
yeye ni waziri?
“Magufuli
hana lolote, msimchague kwa sababu ameshiriki kununua feri mbovu
inayotoka Bagamoyo kwenda Dar es Salaam,” alisema Sumaye.
Katika
maelezo yake, Sumaye alizungumzia pia taarifa za viongozi wa CCM
wanaodaiwa kuwatisha wananchi wasimchague Lowassa kwa kisingizio kwamba
nchi itaingia katika vita kama ilivyotokea Libya na katika nchi nyingine
za Afrika Kaskazini.
Sumaye
alisema hakuna vita itakayotokea wapinzani watakapoingia madarakani na
kwamba vita hiyo itatokea kama Serikali ya CCM haitataka kuondoka
madarakani.
0 comments:
Post a Comment