Musa mateja
POTELEA
mbali! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia wapendanao, mwanamitindo
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba ‘King Kiba’
kuamua kujilipua kwa kuanika hadharani picha zao za kimahaba licha ya
wazazi wa mrembo huyo kutobariki uhusiano huo kwa kigezo cha
kutofautiana dini, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.Hivi
karibuni, ilidaiwa kuwa Jokate alimtambulisha nyumbani kwao lakini
wazazi wake walimchomolea kwa madai kuwa hawaendani kiimani.Jumanne
iliyopita, chanzo chetu kilimtonya paparazi wetu kuwa Jokate ametupia
picha hiyo katika akaunti yake ya mtandao wa Instagram ndipo ‘fasta’
mwanahabari wetu aliposhughulikia ubuyu huo.
“Ametupia
sasa hivi, ingia fasta katika akaunti yake utaona. Inaonesha kabisa
wapo pamoja usiku huu na si ajabu watakuwa nyumbani kwa Kiba Upanga
maana kuna mtu aliniambia huwa mara kadhaa wanalala mpaka asubuhi,”
kilipenyeza chanzo hicho.
Baada ya kuingia kwenye ukurasa huo, mwanahabari wetu aliiona picha hiyo iliyomuonesha Jokate akimbusu Kiba kimahaba hivyo kutoa tafsiri kwamba bado wanaendeleza safari yao ya ‘kimalovee’.Saa chache mbele baada ya kuiweka picha hiyo, mrembo huyo aliitoa hususan baada ya wadau mbalimbali kuanza kumpongeza kwani wamekuwa wakifanya siri sana kuanika penzi lao.
Mwanahabari wetu alipomtafuta Jokate ili kujua sababu za yeye kuweka na kuitoa picha hiyo katika akaunti yake, kama kawaida yake, simu yake iliita bila majibu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu chochote.
Kama ilivyokuwa kwa Jokate, alipotafutwa Kiba naye hakutoa ushirikiano.

0 comments:
Post a Comment