Sunday, September 20, 2015


Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ameponda kauli ya vyama vya upinzani kuwa vitaleta mabadiliko, akisema kazi hiyo tayari imefanywa na CCM.
Akizungumza kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Bukoba wakati wa uzinduzi wa kampeini za wagombea wa chama hicho mkoani Kagera, Mkapa
alisema chama pekee kilichobobea katika ukombozi ni CCM na Serikali zake zilizotangulia.
Kiongozi huyo wa Serikali ya Awamu ya Tatu alisema kuwa lengo la vyama vya upinzani ni kuing’oa CCM na lengo la chama hicho tawala ni kuendelea kushika dola, hivyo upinzani unatakiwa kujifunza hadi baada ya miaka 50. 

1 comment:

  1. Angalia kura ya maoni ya urais Tanzania 2015 hapa: www.mayocoo.com/vote
    Unaweza pia kupiga kura yako ya maoni hapo.

    ReplyDelete