Like Comment
Mtakumbuka hivi karibuni, Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN MBOWE amenukuliwa akisema kuwa chama hicho kina wafadhili watano ambao hatawataja hadharani kwa kuhofia vyombo vya dola kuwafuatilia. Binafsi nilishtushwa sana na kauli hii ya Mbowe na nilijawa na shauku ya kujua ni akina nani hao na kama wanasaidia chama kwa good faith, iweje wafuatiliwe na vyombo vya dola? Mbona Mustapha Sabodo amekuwa akikisaidia chama hicho hadharani na wala hajawahi kuguswa na vyombo hivyo?
Kutokana na kauli hiyo ya Mbowe, kama kawaida yangu niliingia chimbo ili kuwafahamu wafadhili hao na kwa nini Mbowe hataki kuwaweka hadharani.
Wakati nikiendelea na chimbo langu, licha ya kuwabaini wafadhili hao, nimebaini kuwa wafadhili wakubwa wa chama hicho, taasisi ya Ujerumani ya KAS, imesitisha kufadhili chama hicho mara baada ya uamuzi wa CHADEMA kumsimamisha Lowasa kuwa mgombea Urais badala ya Dr Slaa ambaye amefanya kazi na taasisi hiyo kwa muda mrefu. Ni kutokana na hali hiyo, ndipo Mbowe alipomtumia Lowasa kupata wafadhili wa ndani ili kuziba pengo hilo. Wafuatao ni baadhi ya wafadhili hao nami najitolea kuwaweka hadharani.
1. FISADI ROSTAM AZIZ
Huyu ndiye mfadhili namba moja wa CHADEMA kwa sasa. Ufadhili wa Rostam kwa CHADEMA unatokana na uswahiba wake kwa mgombea Urais wa chama hicho, Edward Lowasa. Wawili hawa ni wahanga wa siasa ndani ya CCM na kutokana na jeuri ya pesa waliyokuwanayo ndani ya chama hicho, walidhani kuwa wao ndo kila kitu. Hata walipoambiwa wajivue gamba, Rostam alitii amri ila Lowasa aliendelea kuwa mkaidi kwa kuamini kuwa pengine chama kingelegeza msimamo juu yake.
Kwa sasa Rostam, ametoa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila jimbo ambalo CHADEMA wamesimamisha wagombea Ubunge. Hata hivyo, Rostam hajatoa fedha kwa majimbo ya wabunge wa vyama vingine washirika wa UKAWA. Pia Rostam ametoa dola za Kimarekani milioni 20 ili kufadhili kampeni za Lowasa.
2. FISADI RESERVED
ametokea kuwa na mahaba na CHADEMA kutokana na sababu za kihistoria na kijiografia. Jukumu alilokabidhiwa ni kuhakikisha kuwa Media zote hasa zile za marafiki zao zinakuwa na msimamo wa aina moja huku Lowasa akipewa kavareji ya kutosha kuliko wagombea wengine.
3. FISADI NAZIR KARAMAGI
Naye yupo kwenye hiyo orodha ya Mbowe. Karamagi anashirikiana kwa karibu na akina Hamis Mgeja kuhakikisha kuwa kanda ya Ziwa, Lowasa anapata kura za kutosha. Karamagi ndiye aliyetoa milioni 23 kule Geita wakati wa ziara ya Lowasa mkoani humo ili zitumike kuhamasiaha watu waende kwa wingi kumpokea Lowasa. Kilichotokea ni kwamba watu walikula fedha na hawakufanya kama walivyokubaliana. Pia Karamagi ametoa shilingi kama hizo kwenye mikoa ya Shinyanya, Mwanza, Kagera na Simiyu.
4.RESERVED
Wadau, hawa ndio wafadhili wa Lowasa na CHADEMA. Wengi kati ya hao taswira yao kwenye jamii ni mbaya na ndo maana Mbowe anakuwa na kigugumizi kuwataja waziwazi kwa kuhofia kupoteza idadi kubwa ya wapiga
HAPA KAZI TU.


0 comments:
Post a Comment