Mwenyekiti
Mwenza wa UKAWA Freeman Aikael Mbowe ameshinda rufaa aliyokata Mahakama
Kuu dhidi ya hukumu iliyotolewa katika kesi aliyoshtakiwa kumshambulia
msimamizi wa uchaguzi aliyekuwa akifanya udanganyifu katika fomu za
matokeo ya uchaguzi 2010 huko Hai .Awali Mbowe alihukumiwa faini ya Sh.1,000,000 au kifungo gerezani katika mazingira yanayoonyesha njama za kisiasa na kuzua taharuki kubwa kwa umma.Mbowe alilipa faini kisha akakata rufaa mahakama kuu
Muda mfupi uliopita Mahakama kuu imetengua hukumu na imeamuru arudishiwe fine yake aliolipa.
Kesi hiyo ilikua inasimamiwa na Wakili msomi Peter Kibatala ambaye pia ni Mkurugenzi wa Katiba na Sheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
0 comments:
Post a Comment