MTOTO wa staa naye ni staa! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia kuwepo kwa mipango kabambe ya kufanikisha sherehe ya kumtoa mtoto (arobaini) wa mjasiriamali maarufu Zarinah Hassani ‘Zari The Boss Lady’, Tiffah, Risasi Jumamosi limenasa mchapo kamili.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho ndani ya familia ya Diamond ambaye kwa sasa anaishi pamoja na Zari nyumbani kwake Mivumoni jijini Dar, kumeundwa kamati maalum ambayo inaratibu sherehe hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika Septemba 14, mwaka huu.
“Yaani arobaini ya Tiffah usipime. Shamrashamra tayari zimeanza, wameandaa mambo makubwa kweli siku hiyo. Sare maalum za madera zimeagizwa kutoka India, gharama yake nimesikia ni shilingi laki moja kila moja. Wanatafuta na ukumbi maalum wa kufanyia hafla hiyo baada ya kukamilisha taratibu za kusoma dua nyumbani.
“Kama hiyo haitoshi, ulinzi siku hiyo utakuwa wa nguvu maana kama unavyojua picha ya Tiffah tu ni dili yaani mualiko utatolewa kwa watu maalum pekee,” kilimwaga ubuyu chanzo chetu.
Baada ya kupata ubuyu huo, mwanahabari wetu alimcheki Diamond ambaye alikiri kuwa sherehe hiyo itafanyika na kudai kuwa itakuwa ya tofauti pasipo kufafanua zaidi.
“Yeah itafanyika. Itakuwa ya tofauti kidogo si unajua Tiffah tayari ni staa kwenye mitandao ya kijamii, lazima iwe na hadhi ya kistaa,” alisema Diamond.
0 comments:
Post a Comment