
BI: Anatropia Theonest ambae analalamikiwa na JULIUAS MTATIRO mgombea wa Ukawa jimbo la segerea
NJAMA ZA KUIHUJUMU UKAWA JIMBO LA SEGEREA HAZITAFANIKIWA!!
Nimeshuhudia
mimi mwenyewe jana usiku gari la Matangazo likipita Vingunguti kuhujumu
uzinduzi wa kampeni za UKAWA jimbo la Segerea. Na anayefanya hivyo ni
mwenzangu dada Anatropia Theonest wa
CHADEMA. Ameibuka tena na kutangaza kuwa anazindua kampeni za CHADEMA
katika kata ya Liwiti leo kwa muda na wakati ambapo UKAWA kwa ujumla
inazindua kampeni kuninadi.
Ikumbukwe kuwa dada yetu huyu tayari amepewa barua rasmi na Katibu
Mkuu wa CHADEMA na kujulishwa kuwa mgombea rasmi wa UKAWA ni Julius
Mtatiro (mimi) na aniunge mkono. Na hata baada ya kupewa barua ile
alinipongeza na kusisitiza kuwa tutashirikiana kuiondoa CCM madarakani
na pongezi zake niliziweka hadharani pia.
Nataka
kuwahakikishia wananchi wa Segerea kuwa uzinduzi wetu wa UKAWA uko
palepale, ni LEO JUMAPILI kuanzia saa 7 hadi saa 12 jioni, viwanja vya
Vingunguti Relini. Madiwani wote wa UKAWA watakuwa hapa Vingunguti na
hata viongozi wote wa CHADEMA ngazi ya matawi, kata, jimbo, mkoa na
taifa watakuwa hapa Vingunguti.
Kwa
sababu vurugu hizi anazifanya hadharani na naambiwa anatangaza kuwa ni
bora jimbo liende CCM kuliko CUF kuongoza, nataka yeye na watu wachache
wenye mtizamo huo wajue kuwa UKAWA imejipanga na inaangalia maslahi
mapana ya Segerea na Taifa. Nataka nimwambie mwenzangu kuwa mimi, UKAWA
na wananchi wa Segerea tumepanga kushinda uchaguzi wa mwaka huu na
tutapigana pamoja na kushinda na hata yeye akiendelea kutupinga, anajua
matokeo yake ni nini.
Nimekaa
kimya muda mrefu na sikutaka kumueleza jambo hata alivyokiuka maamuzi
ya viongozi wakuu wa UKAWA ya mgao wa jimbo hili, wakati huo alijenga
hoja kuwa hajapata barua rasmi kutoka kwenye chama chake, chama chake
kimemuandikia barua kutoka makao makuu/Katibu Mkuu - akaipokea,
akaikubali na kunipongeza, siku moja mbele amebadilika, anasema barua
ile ni FEKI. Barua ambayo CHADEMA wameipeleka ngazi zote kuanzia kanda,
mkoa na wilaya hadi jimbo.
Tayari
nafanya kazi na wagombea udiwani wote wa CHADEMA jimbo la Segerea na
wale wa CUF pia, sisi tuendelee na kazi na tumpe dada yetu muda
atafakari hili vurugu analoanzisha lina maslahi ya nani! Ukawa? Segerea?
Taifa? Chadema? Binafsi? Wapambe? CCM? au maslahi ya nani.
UKAWA
jimbo la Segerea tumejipanga kushinda, na tutashinda kwa kishindo. Na
dada yetu akijirudi na kuunga mkono MABADILIKO tutampokea, asiporudi
kundini tutamtakia kila la heri kwenye kampeni zake.
Mtatiro, J,
Segerea - Dar es Salaam,
06 Septemba 2015.
0 comments:
Post a Comment