
Macho
na masikio ya wengi yanaelekezwa kwa wagombea wawili kutoka vyama vikuu
vya siasa, Dk John Magufuli wa CCM na Edward Lowassa wa Chadema, ambao
uchambuzi wa gazeti hili unaonyesha wana mengi yanayoshabihiana.
Wawili
hao ni kati ya makada saba waliosimamishwa na vyama saba kuwania urais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambao
inaelekea kuwa ndiyo watakaochuana vikali, hasa kutokana na ukweli kuwa Dk Magufuli anatoka chama tawala na Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu, anaungwa mkono na vyama vinne vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
inaelekea kuwa ndiyo watakaochuana vikali, hasa kutokana na ukweli kuwa Dk Magufuli anatoka chama tawala na Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu, anaungwa mkono na vyama vinne vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Wengine
wanaowania urais ni Mchungaji Christopher Mtikila wa DP, Chifu Lutayosa
Chemba (ADC), Macmillan Limo (TLP), Hashimu Rungwe (Chauma), Fahami
Dovutwa (UPDP) na mgombea wa ACT Wazalendo ambaye bado hajateuliwa.
Pamoja
na kwamba katika siasa lolote linaweza kutokea, wagombea hao watano
hawatazamiwi kuweka ushindani mkubwa zaidi ya ule wa Dk Magufuli na
Lowassa.
Dk
Magufuli hakutarajiwa kupita kwenye mbio za urais ndani ya CCM, ambako
Lowassa na vigogo wengine walikuwa wakipewa nafasi kubwa, lakini ushindi
wake umemfanya awe mgombea wa chama chenye mtandao mkubwa nchini na
hivyo mwanzoni kupewa nafasi kubwa ya kushinda.
Hata
hivyo, uamuzi wa Lowassa kujivua uanachama wa chama kilichomlea na
kilichompa umaarufu mkubwa, umebadili upepo na sasa vita ya kuingia
Ikulu Oktoba 25 inaonekana kuwa ya watu hao wawili.
Gazeti
la Mwananchi linaangalia sifa ambazo wawili hao wanashabihiana pamoja
na tofauti zao, kwa kuzingatia maelezo ya wachambuzi wa masuala ya
kisiasa.
Wote wamesomea ualimu
Moja
ya mambo ambayo wawili hao wanashabihiana ni kusomea ualimu, ingawa wa
fani tofauti. Dk Magufuli, ambaye atakuwa akitimiza miaka 56 siku nne
baada ya Uchaguzi Mkuu, ni mwalimu aliyejikita kwenye masomo ya kemia na
hesabu.
Alipata
diploma ya ualimu mwaka 1982 kwenye Chuo cha Elimu Mkwawa, kabla ya
kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alipata shahada yake ya
kwanza, ya umahiri na ya uzamiri akijikita kwenye somo la kemia.
Lowassa,
ambaye Agosti 26 atakuwa akitimiza miaka 62, alisomea shahada ya ualimu
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1977, lakini shahada yake ya uzamili
ilijikita kwenye masomo ya maendeleo ya jamii.
Dk
Magufuli alitumia taaluma yake kufundisha kemia na hesabu kwenye Shule
ya Sekondari ya Sengerema, lakini Lowassa hakufundisha.
Wote ni makini
Pengine
ni kutokana na maadili ya ualimu, wawili hao wamedhihirisha kuwa ni
watu makini katika utendaji wao, jambo ambalo limekuwa likiwafanya watu
wanaofanya kazi chini yao kuwa na wasiwasi kila wanapowapeleka taarifa.
Dk
Magufuli na Lowassa hutumia muda mwingi kujiridhisha na taarifa
wanazopelekewa kabla ya kufanya uamuzi ambao wakati mwingine huonekana
kama wamekurupuka.
Mhandisi
mmoja ambaye amewahi kufungiwa leseni na Magufuli aliiambia Mwananchi
kuwa kosa moja kubwa alilofanya ni kumwandikia Dk Magufuli taarifa
ndefu, lakini iliyojaa mambo yasiyo sahihi.
Anasema kuwa aya hiyo ilikuwa ukurasa wa 20, lakini ndani ya muda mfupi Magufuli aliibaini na kibarua chake kiliota nyasi.
Hali
ni kama hiyo kwa Lowassa, ambaye akiwa Waziri Mkuu aliwahi kumtimua
mkandarasi wa Wilaya Temeke kwa kushindwa kukagua ujenzi wa maghorofa
ikiwemo la Chang’ombe Village lililoporomoka na kusababisha maafa ya mtu
mmoja na wengine kadhaa kujeruhiwa mwaka 2006.
Uchapakazi
Mbali
na umakini, wawili hao wamedhihirisha kuwa ni wachapakazi hodari katika
wizara na taasisi walizopitia kiasi cha kujijengea jina kubwa kwa
wananchi.
Utendaji
wa Dk Magufuli hauna shaka na ameshaeleza bayana kuwa hapendi wazembe
na wasiowajibika sanjari, kama Lowassa ambaye hata siku ya kwanza
alipoingia ofisini mwaka 2005 aliwataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Wakati
Dk Magufuli alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wengi walidhani
kuwa amemaliza kisiasa, lakini mbunge huyo wa Chato alifanya kazi kubwa
ya kutambua fursa za kiuchumi zilizoko hasa kwenye uvuvi na akafanikiwa
kuonyesha ni kiasi gani Serikali ilikuwa ikipoteza fedha.
Wakati
huo, Tanzania iliingia makubaliano na Afrika Kusini na nchi nyingine za
ukanda huu kufanya doria kwa pamoja kwenye pwani ya Afrika Mashariki na
juhudi hizo zilifanikiwa kunasa meli ya Tawaliq 1 iliyokuwa na samaki
wenye thamani ya Sh20 bilioni.
Uchapakazi
wake umedhihirika hasa kwenye ujenzi wa barabara, akiwa amefanikiwa
kuunganisha takriban mikoa yote ya Tanzania katikja kipindi alichokaa
Wizara ya Ujenzi.
Lowassa
anaonekana zaidi katika kusimamia utekelezaji wa mradi wa maji ya Ziwa
Victoria katika shughuli za maendeleo baada ya mpambano mkali dhidi ya
Misri, ambayo ilikuwa na ukiritimba wa maji hayo kabla ya nchi tano
kuungana na kusaini makubaliano ya matumizi ya maji hayo.
Lowassa
pia anajinadi na mafanikio ya ujenzi wa shule za kata, ambazo kwa kiasi
kikubwa zimefanikisha watoto wengi kupata elimu kwa gharama nafuu,
ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma ambao aliufanya kwa kukutanisha mifuko
ya hifadhi ya jamii na kuiamuru ichangia gharama za ujenzi.
Jambo
lingine walilonalo Dk Magufuli na Lowassa ni misimamo. Dk Magufuli ni
kiongozi mwenye misimamo isiyotia shaka na siku zote husimamia
anachokiamini, sanjari na Lowassa, ni mwenye misimo yake na itakumbukwa
alipokuwa Waziri wa Maji na baadaye Waziri Mkuu alionyesha misimamo.
Dk
Magufuli alitofautiana hata na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati
aliposimamia uendeshaji wa kivuko cha Kigamboni, na suala la kiwango cha
mizigo inayobebwa na malori.
Moja
ya kauli zilizonukuliwa sana ni ile ya “asiyekuwa na nauli ya kulipia
kivuko, apige mbizi”, ambayo ilitafsiriwa kuwa ya kutojali wananchi,
lakini faida zake ndio zinamfanya aonekane kuwa msimamo wake ulilenga
kunufaisha wananchi.
Hali
kadhalika Lowassa anajulikana kwa kusimamia uamuzi kama wa kubomoa
maghorofa yaliyojengwa kinyume na sheria Masaki jijini Dar es Salaam.
Msimamo wake pia kwenye suala la mkataba wa City Water iliyokuwa
ikihusika na ugavi wa maji jijini Dar es Salaam ndio uliosababisha
uvunjwe.
Ufuatiliaji
Lowassa
na Dk Magufuli pia wanajulikana kwa kuwa wafuatiliaji wazuri kwa watu
walio chini yao au wanaofanya kazi chini ya mamlaka zao. Dk Magufuli,
ambaye anajulikana kwa kukariri tarehe, kiwango cha miradi, urefu wa
barabara na kiwango cha fedha zilizotengwa kwenye miradi, hutumia
talanta hiyo kufuatilia miradi mbalimbali na hasa muda wa kumalizika,
hali inayomfanya kila mara atishia kuvunja mikataba na wakandarasi au
kuivunja kabisa.
Hilo
pia limekuwa likifanywa na Lowassa, ambaye akiwa Waziri Mkuu alikuwa
akihakikisha wakuu wa wilaya na mikoa wako sehemu zao za kazi na yeyote
ambaye alitaka kutoka alitakiwa awe na kibali, kwa mujibu wa baadhi ya
watu waliofanya kazi naye.
Udhaifu
Mbali
na sifa hizo nzuri, wanasiasa hao wanashabihiana katika udhaifu, hasa
uamuzi wa papo kwa papo ambao pia husababishwa na kiu yao ya kutaka
kuona kazi inafanyika.
Wote
wawili hufanya uamuzi wa papo kwa pamo ambao wakati mwingine huwa na
athari za kisheria. Uamuzi kama huo huwa na kadhia kwa wafanyakazi na
makandarasi wanaopewa zabuni mbalimbali na Serikali.
Hawaachi mfumo wa utendaji
Udhaifu
mwingine wa wawili hao ni hali ya kujituma wao bila ya kutengeneza
mfumo ambao unaendeleza ufanisi na badala yake wanapoondoka, hali
hubakia kama ilivyokuwa awali.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Dk Magufuli kwenye wizara alizopitia kama ya uvuvi na hali kadhalika kwa Lowassa.
Pia wanatofautiana
Tofauti
kubwa kati ya Dk Magufuli na Lowassa ni mgombea huyo wa CCM kutokulia
ndani ya chama na badala yake amekuwa kwenye nafasi za utendaji zaidi na
uwaziri. Dk Magufuli amekuwa mwanachama wa CCM na mbunge, nafasi ambayo
humuingiza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu pekee.
Lakini Lowassa ameshika nafasi mbalimbali kwenye chama kuanzia katibu wa mkoa hadi mjumbe wa vyombo vya juu vya CCM.
Kauli za wachambuzi
Baadhi
ya wachambuzi na wasomi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (Udsm)
wamesema kwa nyakati tofauti kwamba wagombea hao wanaonekana kuwa na
tofauti kubwa zinazoweza kufanikisha ushindi katika uchaguzi huo.
Mohammed
Bakari, ambaye ni mhadhiri wa Idara ya Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, alisema wagombea hao wanafanana katika kigezo cha
utendaji kazi lakini kiuamuzi na uzoefu wanatofautiana.
“Dk
Magufuli ana uamuzi wa kukurupuka ila Lowassa ametulia,” alisema.
“Kuhusu uzoefu pia Lowassa ni mzoefu kiuongozi kuliko Dk Magufuli.”
Alisema
suala la uadilifu siyo rahisi kupata kiongozi mwadilifu kwa wagombea
hao na bila kuzitaja kashfa hizo, alisema wote wana kashfa. Aliongeza
kwamba, Lowassa ni mgombea anayeweza kuleta mabadiliko kwa Taifa hili,
lakini Dk Maghufuli hawezi kutokana na mfumo uliopo kwenye chama chake.
Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa wa Udsm, Dk Alexander Makulilo pia anaona sifa hizo zinazolingana.
Alisema
wagombea hao wanafanana kwa utendaji mzuri wa kazi na uamuzi wa papo
kwa hapo. Aidha, alisema Magufuli ni kiongozi anayeweza kuleta siasa
mpya zisizokuwa na makundi.
Alisema
Lowassa ni mgombea anayekabiliwa na changamoto ya Richmond iliyomfanya
ajiuzulu uwaziri mkuu, wakati Dk Magufuli hana kashfa kubwa iliyowahi
kujadiliwa bungeni.
“Lakini
hali hiyo haiwezi kuwa changamoto kubwa kutokana na mwamko mkubwa wa
kundi linalohitaji mabadiliko ya uongozi serikalini. Uchaguzi huu
ninaufananisha na Zambia wakati chama cha UNIP kilipoondolewa madarakani
kwa kuwa makundi ya kijamii yalikuwa yameamua kiondoke madarakani,”
alisema.
Kuhusu
mfumo kuibeba CCM, Dk Makulilo alisema ni sehemu ya changamoto kubwa
inayoweza kufanikisha ndoto za Lowassa kuingia madarakani.
MAKALA hii ni sehemu ya makala ya gazeti la Mwananchi 8.82015
she is beautiful
ReplyDeleteMi ni mmojawapo wa watu wasiokuwa na ushabiki wa vyama vyovyote vya siasa, na kwamba nakiri sijapiga kura miaka mingi, vile nilikuwa naamini maendeleo yangu binafsi na ya familia yangu pamoja na kuwa yanaletwa na serikalini, lakini jitahida zangu na bidii ndiyo zinazoniketea maendeleo. Lakini sikupendezwa na kashfa za uchotwaji ws mahela ya serikali iliyopo chini ya CCM. Na nilikuwa nafarijika vyama vya upinzani kurekebisha serikali. Hivyo nilitarajia kuwa bunge hili kuwa xuri zaidi.
ReplyDeletelakini baada ya chadema kumchukua lowasa awe mgombea urais, mwaka huu ntapiga kura, na ntamchagua magufuli. Na ninamuombea kws mungu achaguliwe kwa percent 100.
Hivi utategemeaje lowassa alete mabadiliko, lowasa ataanzaje kuwakemea mafisadi, na yeye alikuwa kinara wa mafisadi, hainiingi akilini kwa chadema kumchukua lowassa kama mgombea urais wao. Kweli lowassa katika kambi ya upinzani anaweza kuikemea serikali iliyoko madarakani. Jamani tufikirie siku tutakapoenda kupiga kura, tusiwape nchi watu watakaokuwa wanajichotea tu utajiri wetu kunufaisha marafiki zao. Marafiki wa lowasa akina Rotam, jamani mmetula vya kutodha hamuoni aibu, tuachieni basi angalau tuweze kupewa panadol tukienda hosp.
mtanzania halisi