Friday, September 4, 2015



UKAWA YA 2015 SIO KAMA NARC YA KENYA YA 2002…

Wapo watu wanaosema, mwaka huu 2015 UKAWA itaiondoa CCM madarakani kama umoja (coalition) wa NARC nchini Kenya ulivyoindoa chama cha KANU mwaka 2002.


Hizo ni ndoto za mchana (day dreaming).  Nitatoa tofauti kubwa 4 kati ya UKAWA TANZANIA 2015 na NARC UKAWA 2002

1. UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU

Mwaka 2002 nchini Kenya kulikuwa na kambi 2 kubwa yaani KANU na NARC. Wapinzani wote waliamua kuungana.

 Nchini Tanzania, vyama vya upinzani havijaungana. UKAWA haiwakilishi upinzani wote wenye vyama 21 vyenye usajili wa kudumu. Kambi ya ukawa in vyama vi-4 tu ambayo ni 19%.

Nchini Tanzania jumla ya wagombea urais ni 8.

2. UROHO WA MADARAKA

Mwaka 2002, Raila Odinga wa Kenya alijiondoa chama cha KANU muda mfupi kabla ya uchaguzi. Alijiondoa baada ya Uhuru Kenyatta kupendelewa na rais Daniel arap Moi na kufanywa mgombea urais wa KANU.

Raila akajiunga na umoja (coalition) wa NARC. Lakini kwa jinsi asivyo mbinafsi na mroho wa madaraka, hakuwa mgombea urais. Yeye akamuunga mkono Mwai Kibaki. Akazunguka nchi nzima akisema “KIBAKI TOSHA”.

UKAWA ni tofauti. ALIYEKATWA CCM kwa matatizo ya maadili ndio amefanywa kuwa mgombea urais.

3. NGUVU YA CCM, UDHAIFU WA KANU

Chama cha KANU tayari kilishaonyesha kuwa na udhaifu mkubwa wa kisiasa kutokana na asili ya siasa za ukabila nchini Kenya na utendaji mbovu wa chama hicho. Tokea uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1992 kilikuwa kinashinda kwa asilimia chache sana (chini ya 40%).

Nchini Tanzania CCM ni chama imara nchini kote. Nchini Tanzania hakuna changamoto ya ukabila. CCM ina mtandao mpana wa wanachama. Kihistoria hakijawahi kupata kura chini ya 61%.

Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 CCM ilishinda kwa zaidi ya 80%.

- So uwezekano wa UKAWA muungano wa vyama 4 vya siasa Tanzania wenye Wanachama MILLIONI 2 NA 1/2 kukishinda CCM chenye Wanachama Millioni 8 ni absolutely impossible kuna makelele ya mtaani na ukweli halisi, UKAWA hawana nambaz za kushinda CCM wanazo. 

Le Mutuz Nation


0 comments:

Post a Comment