•Katika nchi ya Marekani (kwa mfano wa jambo ninalotaka
kulielezea) kuna maeneo ambayo kwenye chaguzi zote huchagua chama cha
Republican. Majimbo haya huitwa “stronghold” yaani ngome ya Republican.
•Kuna majimbo ambayo, kwa sababu za kihistoria, karibia
chaguzi zote huchagua Democrats. Hii huitwa “stronghold” (ngome) ya Democrats.
•Kuna majimbo ambayo. Haya huitwa “Swing States”. Haya
ndio mara nyingi huamua mshindi. Majimbo haya mara nyingi huwa na wapiga kura
wanaoitwa “undecided voters”. Kwa majimbo haya, watu wengi hupiga kura kutokana
na mazingira ya kisiasa ya mwaka huo.
•Nchini Tanzania kuna majimbo na ngome kadhaa kwa jinsi
kanda tofauti za mikoa zinavyoweza kugawanywa .
•Ili chama kishinde ni lazima kiwe na ngome za kutosha.
•Kwa mfano, kila mtu anajua, ngome ya chama cha CUF ipo
kwenye eneo dogo sana la Pemba. Hili ni eneo dogo sana. Halitoshi kuleta ushindi.
Ndio maana mgombea urais wa CUF, Ubrahim Lipumba mwaka 2010 alipata kura kama
469,780 ambayo haifikii hata idadi ya mabalozi wa shina (mabalozi wa nyumba
kumi kumi) wa CCM ambao ni zaidi ya 600,000. Eneo hili dogo la Pemba hivi sasa
CUF imepata mshindani mpya ambaye ni ADC.
•CUF ni chama chenye wabunge wawili tu Tanzania Bara
yaani Lindi Mjini na Kilwa Kusini.
• Chama cha NCCR Mageuzi kwa karibia miaka 10 kilikuwa
hakina mbunge hata mmoja. Mwaka 2010 kilipata wabunge wa-4 wote kutoka mkoa wa
Kigoma pekee. Lakini cha kushangaza, kwenye matokeo ya urais, mgombea urais wa
NCCR-Mageuzi, Hashim Rungwe, hakupewa kura nyingi mkoani Kigoma ukifananisha.
Kwa hiyo hii sio ngome ya NCCR-Mageuzi. Na mwaka huu, uwepo wa ACT Wazalendo,
utaiondoa NCCR Mageuzi kwenye ramani.
•Ngome pekee ya UKAWA kwa hivi sasa, ngome ya CHADEMA ambayo
ni mikoa ya KASKAZINI kwa maana ya Kilimanjaro na Arusha.
• Hii haijatokea kwa bahati mbaya. Hii ina uhusiano
mkubwa na asili ya waanzilishi wa chama. Mwenyekiti wa chama, mgombea urais wa
chama na wafadhili wakubwa wa chama wote wanatokea ukanda huu.
•Watu wote ni mashahidi. Katika kipindi cha miaka mi-5
yaani 2010-2015, matukio mengi ya maandamano na mikutano ya CHADEMA imekuwa
ikifanyikia katika jiji la Arusha kuliko sehemu yoyote nyingine ya nchi hii.
Mikutano na maandamano haya wakati mwingine imeleta hadi maafa.
•Ngome nyingine zote zilizobaki ni za CCM. Katika ngome
hizo za CCM, inaweza kutokea sehemu moja moja (hususan mijini) ambako upinzani
ukawa maarufu zaidi. Kwa mfano mkoa wa Iringa kunaweza kuwa na kura nyingi za
upinzani kutoka Iringa mjini. Lakini ukichukulia ujumla wa mkoa wote na majimbo
yake yote, lazima kura nyingi zitakuwa ni za CCM.
•Hizi
zote ni ishara ya ushindi wa mapema asubuhi kwa CCM, moja ya vyama vikongwe
zaidi barani Afrika.
Le Mutuz Nation

0 comments:
Post a Comment