Friday, September 11, 2015


Imelda Mtema
MWANADADA aliyejipatia jina kupitia Shindano la Maisha Plus Season 11, Jack Dustan amejikuta akiihama nyumba aliyokuwa amepanga maeneo ya Shekilango jijini Dar, kwa madai kwamba ilikuwa na nguvu za kishirikina ‘mapepo’.
Akistorisha na Amani hivi karibuni, Jack alisema nyumba hiyo alipanga na kukaa kama wiki moja tu lakini akawa anakumbwa na mambo ya ajabu kwani kuna wakati alikuwa akijikuta amelala nje kwenye kizingiti cha mlango wa chumbani kwake.
Aliendelea kusema siku aliyoamua kuondoka bila kubeba vitu vyake vya ndani ni baada ya usiku kupigwa sana vibao na kuamriwa kutoa pombe alizoweka kwenye kabati ili awe salama.
“Ukweli sijabeba kitu chochote, nilitimua zangu usiku uleule na kwenda kulala kwa rafiki yangu na nimetafuta nyumba nyingine-,” alisema Jack.

0 comments:

Post a Comment