“Kusema kweli tunathubutu kufanya show kipindi cha uchaguzi kwasababu kwetu muziki ni ajira ni kazi yetu…Hatuwezi kusitisha kile ambacho kinatuletea mkate,” alisema Vanessa kupitia 255 ya XXL.
Vee Money hakusita kuwashauri wasanii wengine ambao wamesitisha kufanya kazi zao katika kipindi hiki cha uchaguzi.
“Ningewasihi wasanii wengine wasiogope kufanya vitu katika kipindi hiki kwasababu kama ni ajira yako hutakiwi kuacha kufanya katika kipindi hiki, kitu kikubwa zaidi siku ya kupiga kura wote tuunganike kama Watanzania tukapige kura.”
Kupitia Instagram Jux pia alishare picha na kuonesha kinachoonekana kuwa mavuno ya show ya Mbeya na kuandika:
“Asanteni mbeya kwa upendo wenu #africanboy I ain’t walking for no cheesecake #mbeyamoney #goodmusicfamily we coming to your city soon”
0 comments:
Post a Comment